PYONYANG, Majasusi wa Korea ya Kusini na Marekani wamethibitisha kuwa,silaha mpya ya kimkakati iliyotajwa na kiongozi wa Jamhuri ya Watu wa Kidemokrasia ya Korea, Kim Jong Un mwishoni mwa mwaka jana tayari imeundwa na inaonyesha kuwa ni tishio la usalama.
Wamesema,manowari mpya ya tani 3,000 yenye vifaa vingi vya makombora imezinduliwa na kikosi maalum cha SLBM.
Kwa mujibu wa Gazeti la The Dong-a Ilbo linalochapishwa nchini Korea Kusini limedai katika ripoti yake kuwa, Korea Kaskazini imeshafanikiwa kuunda makombora hayo ya balestiki ambayo yanatwajwa kuwa ya masafa marefu yenye uwezo wa kupaa kutoka bara moja hadi jingine.
Gazeti hilo lilifafanuwa kuwa, makachero wa Marekani na Korea Kusini wamenasa taarifa za kiintelijensia zinazoonyesha kuwa, Korea Kaskazini imefanikiwa kutengeza na kukamilisha uundaji wa makombora hayo katika kiwanda kimoja cha utengezaji makombora kilichopo mjini Shinpo katika Jimbo la Kusini la Hamgyong. Zaidi soma Gazeti la Majira popote ulipo Tanzania
More Stories
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best
Waziri Mavunde:Benki Kuu yanunua tani 2.6 za Dhahabu nchini
Kampeni msaada wa kisheria ya mama Samia kutatua kero za kisheria Katavi