December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kilimo cha bangi ruksa kwa ajili ya kisayansi

Na Doreen Aloyce, TimesMajira Online, Dodoma

MAMLAKAya ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya nchini imesema inaweza kuruhusu kilimo cha bangi kwa ajili ya matumizi ya kisayansi na dawa, lakini si vinginevyo.

Akizungumza leo jijini hapa, Kamishna wa Tiba na Kinga wa Mamlaka hiyo, Dkt. Peter Mfisi, amesema wanaweza kuruhusu kilimo cha bangi na Coke kwa ajili ya dawa na matumizi ya kisayansi.

“Kilimo cha bangi tunaweza kuruhusu kwa ajili ya watu wanaolima kwa ajili ya kisayansi,dawa au utafiti lakini si vinginevyo,” amesema Dktk. Mfisi.

Aidha Kamishna huyo amesema hata kama wataruhusu mtu kulima bangi, lakini lazima wawe na uthibitisho wa matumizi yake kwani hawataruhusu watu watumie mmea huo kwa kustarehe.

Hata hivyo, Dkt. Mfisi amesema mpaka sasa hakuna mwekezaji yeyote aliyeenda kuomba kibali cha kulima bangi kwa ajili ya matumizi hayo, licha ya kuwa sheria inaruhusu.

Wakati huo huo Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge, Kazi ajira,Vijana Ulemavu na Watu wenye Ulemavu, Antony Mavunde amesema Serikali kupitia Mamlaka hiyo imepata mafanikio makubwa katika mapambano ya kudhibiti dawa za kulevya katika kipindi cha mwaka 2019.