November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kikwete atembelea kampuni ya Raphael Group kuona uzalishaji

Na Esther Macha,Timesmajira Online, Mbeya

RAIS Mstaafu wa Awamu ya Nne Jakaya Mrisho Kikwete na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la AGRA ametembelea na kuona shughuli za uzalishaji  na usambazaji wa nafaka mbali mbali  wa Kampuni ya Raphael Group  iliyopo eneo la Uyole Jijini Mbeya  na kuwataka kuongeza tija  na kuwepo kwa chakula cha ziada .

Kikwete amesema hayo jana wakati alipotembelea kampuni hiyo kwa lengo la kuona shughuli za uzalishaji za kampuni  hiyo ambazo ni ukoboaji mpunga,uandaaji na ufungashaji, kilimo cha mkataba  na wakulima , ukamuaji wa mafuta ya alizeti ununuzi wa uchataji mahindi  ununuzi na uuzaji wa mchele  , uuzaji wa maharage,uuzaji mtama na Soya  pamoja na uzalishaji mwingine.

Aidha Kikwete amesema  katika kuona wakulima kuzalisha  mazao   ya kimkakati wanatoa  mafunzo kwa  wataalamu  kupitia Agra katika shahada ya uzamili na nyinginezo  lengo ni kuona wakulima wadogo na kwa   Tanzania wamezalisha  wataalam 42 wataokaosaidia  katika Sekta ya Kilimo.

Kwa upande wake mkurugenzi wa Raphael Group ,Raphael Ndelwa amesema kuwa baada ya kujiirimarisha vyema katika  shughuli kampuni hiyo iliona fursa  za kufanya kazi na wakulima wadogo wadogo ili kujihakikishia upatikanaji wa malighafi  wa mazao zinazotakiwa kwa wingi , ubora kwa wakati muafaka.

Ndelwa amesema kuwa kwa madhumuni hayo  kampuni hiyo  ilianza kufanya kazi na wakulima wa mazao  moja kwa moja mwaka 2010 ambapo  kipindi chote  cha  nyuma  ili kutegemea ununuzi wa mazao kutoka kwa wanunuzi wa kati .

Aidha Mkurugenzi huyo amesema kuwa  mpaka sasa  kampuni hiyo inafanya kazi kwa mfumo wa kilimo cha mkataba na wakulima zaidi ya 15,000 ambao wamejiajiri katika kilimo  ambapo wakulima wa mpunga ni 10,000 na wakulima wa Maharage  zaidi ya 5,800.

Katika ziara hiyo, Rais mstaafu Kikwete amefuatana na Naibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde pamoja na viongozi wa shirika la AGRA  na Britten.