Na Mwandishi Wetu,
RAIS Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amekutana na kufanya mazungumzo na Ban Ki-moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mstaafu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Ban Ki-moon jijini Seoul, Korea Kusini leo.
Dkt. Kikwete, ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya  Taasisi ya Kimataifa inayoshughulikia Masuala ya Elimu Duniani (Global Partnership for Education) – GPE) yuko Seoul, Korea Kusini kwa ajili ya kukutana na viongozi wa Serikali na Mashirika Mbalimbali ya Korea Kusini kwa ajili ya kujadili mikakati ya kuendelea kuboresha elimu katika nchi zinazoendelea. GPE ambayo ilianzishwa na nchi za G7 miaka 20 iliyopita, imeendelea kupigania elimu kwa ajili ya mtoto wa kike na wa kiume kwa kuomba kuungwa mkono na nchi na taasisi zinazoweza kuchangia katika elimu duniani.
More Stories
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini
Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi watakiwa kusimamia programu za chakula shuleni
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano