March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kikwete aipongeza Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa kuwajengea uwezo Wakuu wa Taasisi,Mashirika na Wakala wa serikali

Na Bakari Lulela,Timesmajira

Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri mkuu (kazi, vijana, ajira na wenye Ulemavu) Ridhiwani Kikwete ameipongeza Ofisi ya msajili wa hazina kwa kuwapa Mafunzo  wezeshi ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji wakuu wa taasisi, Mashirika na wakala wa serikali ili waweze kuleta tija maeneo yao ya kazi.

Akizungumza wakati akifunga Mafunzo ya siku tatu katika chuo cha uongozi kibaha mkoani Pwani waziri huyo amesema kuwa Mafunzo hayo yatawasaidia kuboresha utendaji wenu na mikakati  mbalimbali kwa kuzingatia weredi na ufanisi sehemu za kazi.

“Wakuu wa taasisi, Mashirika na wakala  wapatao 114 wamepatiwa Mafunzo haya, ambapo wayachukulie kama nyenzo ya kuleta mabadiliko chanya katika utendaji wa majukumu yenu,” amesema Kikwete 

Aidha Kikwete ameeleza kuwa lengo la Mafunzo hayo ni kuwaimarisha wakuu hao Ili waweze kuimarisha sekta ya uongozi kwenye maeneo yao ili kuongeza tija katika uzalishaji mali.

Waziri huyo amesema Mafunzo hayo yaweze kuwa chanzo cha mabadiliko  katika mifumo kandamizi ya kiutendaji na kuongeza fursa za upatikanaji wa ajira kwa watanzania.

Kwa kuzingatia weledi wa majukumu yenu ,na tukumbuke kumuunga mikono Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassani katika kushiriki uchaguzi mkuu ambao unatarajia kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

Kwa upande wake Msajili wa Ofisi ya Hazina Nehemiah Mchechu ameshukuru waziri wa nchi Ofisi ya Waziri mkuu (kazi, vijana, ajira na wenye Ulemavu) kwa kuacha majukumu yake na kuungana nae kwenye hafla ya utungaji wa Mafunzo hayo.

Mchechu amesema Mafunzo yalikuwa na lengo la kuwajengea uwezo na maarifa wakuu wa taasisi, Mashirika Ili kuweza kukabiliana na majukumu mbalimbali ya Ofisi zao.

Hata hivyo Mafunzo haya yatawasaidia wakuu hawa kuchochea fursa za uzalishaji bora na utendaji ulitukuka maeneo yao ya kazi bila kubagua jinsia zao wala dini zao.

Ameendelea kwa kusema Mafunzo hayo ni matokeo kwa wakuu hawa kufanya kazi kwa ushindani Ili kuongeza fursa za uwekezaji maeneo mbalimbali ya nchi yetu.