Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
MSANII Mkongwe hapa nchini katika muziki wa Bongo fleva Joseph Haule maarufu kama ‘Professor Jay’, amekasirishwa na ‘Kiki’ wanazozitafuta wasanii wa sasa badala ya kushindana kwenye muziki lakini matokeo yake wanarumbana kwenye mitandao ya kijamii kwa maneno machafu jambo ambalo linachangia kuua mziki wa Tanzania.
Akizungumzia hilo, Professor Jay amesema siku zote Muziki unaongea, hivyo huwa anapata hasira kuona yale waliyopigania (Muziki) hayaongei, kinachoongea ni Kiki.
Professor Jay amesema, kutokana na yanayoendelea sasa (kiki na kashfa kuliko muziki), muziki wa Tanzania unashuka. Kwani miaka michache nyuma walikuwa wanashindana na wanamuziki wa Nigeria, na mataifa mengine lakini kwa sasa wao (kina Davido , Wizkidayo na wengine) wanapambania Grammy na tuzo nyingine za Kimataifa, huku Tanzania wanapambania Kutrend kwenye Youtube na Instagram.
Amesema, hao ambao wanafurahi wanayofanya kwa sasa, kuna siku watashuka na walalamike kwamba wamerogwa wakati walijiroga wenyewe.
More Stories
GETHSEMANE GROUP KINONDONI yaja na wimbo wa siku yetu kwaajili ya harusi
Startimes yazindua makala ya China, Africa
Mwanasheria wa Katavi aliyetimkia kwenye muziki achaguliwa tuzo za MIEMMA