Na Bakari Lulela, TimesMajira Online
KAMPUNI ya Vijana Real Estate imemtangaza Mtangazaji nguli wa Kimataifa Salum Kikeke kuwa Balozi wao hususan katika mradi wao mpya ambao upo Msoga Kibaha mkoani Pwani.
Mkurugenzi wa Vijana Real Estate, Daudi Hazaidu, amesema lengo la kumpa ubalozi huo ni kuhakikisha wanapata wateja wengi WA kitanzania waliopo nje ya nchi.
“Kuna watanzania wengi ambao wapi nje na wamekuwa wakituma fedha kwa ndugu ama jamaa zao wawatafutie viwanja na wengi wao wamekuwa wakitapeliwa hivyo changamoto hiyo tunakwenda kuimaliza,” amesema Hazaidu
Pia amesema kuwa hata kwa wateja walioko nje ambao watanunua kiwanja na kutaka kujengewa nyumba wao wanafanya ili kuhakikisha wanasaidia watanzania kuwa makazi.Â
Katika utambulisho huo wa Balozi wa kampuni hiyo, pia walitoa zawadi ya viwanja viwili kwa wateja wawili ambao walitoa comment katika akaunti yao ya Facebook.Pia Hazaibu, amesema kuwa waandishi wa habari wanakaribishwa kununua viwanja hivyo kwa punguzo la sh. 1,200,000 badala ya 1,500,000.
Aliongeza wateja wanaweza kununua viwanja hivyo kwa kulipa kidogokidogo kwa kipindi cha mwaka mmoja ambapo utakabidhiwa kiwanja hicho kwa utaratibu mzuri.
Naye Kikeke amesema kuwa anashukuru kupata nafasi hiyo kwani wakati anarejea nchini moja ya lengo lake ni kuhakikisha anafanya kazi na vijana hivyo ni fursa pekee ambayo anajivunia.Pia Kikeke amesema kuwa viwanja hivyo kutoka Dar es Salaam ni dakika 40 na kutoka kituo cha SGR ni umbali wa km mbili.
Pia kwa wateja wetu, wakati wa kwenda Soga wanaweza kutumia usafiri treni SGR ama barabara na kuwaomba watanzania wajitokeze Kwa wingi kununua viwanja hivyo.
“Ni mradi mzuri sana na unapokuwa katika mradi huo, unaona treni za umeme na Kwa taifa lolote ambalo linaendeleo hayo ni maeneo sahihi ya kuishi,” amesema.
Happynes Mbise, Meneja Masoko wa kampuni hiyo, amesema Lengo la kupeleka mradi huo Soga ni kusapoti miradi mbalimbali inayofanywa n Rais Dk Samia Suluhu Hassan katika kuinua uchumi wa nchi na kuwaletea watanzani maendeleo.
More Stories
TTCL yafanya maboresho katika huduma zake
HGWT yawataka wazazi na walezi kulinda watoto dhidi vitendo vya ukatili
ACT-Wazalendo,waitaka Polisi kutobeba chama kimoja