Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online. Shinyanga
KATINU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Kenani Kihongosi, amesema chama hicho kipo imara kuanzia ngazi ya matawi hivyo amewataka wanachama wake kutembea kifua mbele.
Pia amewasisitiza wanachama wa Shina namba tatu la tawi la Bushushu lililopo kata ya Lubaga mkoani Shinyanga na watanzania kwa ujumla kuendelea kulinda amani, kupendana, kudumisha umoja na mshikamano ndani na nje ya chama.
Kihongosi amesema hayo Machi 6, 2026 alipotembelea Shina namba tatu la tawi la Bushushu lililopo kata ya Lubaga mkoani Shinyanga, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kichama akiendelea kukagua uhai wa chama, utekelezaji wa Ilani ya CCM na kusikiliza na kutatua kero za wananchi.
Amesema vyama vingine vingi vinekuwa vikishangaa kuhusu ushindi wa CCM bila ya kujua kuwa uhai na ushindi wa vyama vya siasa hutokana na mashina.
“Vyama vingi vya siasa havina mashina na huwa vinashangaa CCM imeshindaje?.Wakati CCM ina uongozi kuanzia kwenye mashina.
Akisoma taarifa ya Shina, mmoja wa wanachama Paulina Jeremia amesema, shina hilo lilianzishwa Aprili 29, 2004 likiwa na wanachama 26, ambapo hivi sasa wamefikia wanachama 87, huku akimuomba Katibu huyo, kusaidia nyumba ya mwenyekiti wao, Boniface Mtende ipate umeme.
Aidha, Kihongosi alimuelekeza msaidizi wa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, kuwasiliana na TANESCO ili taratibu za nyumba hiyo kuingizwa umeme zianze..
Kihongosi yupo mkoani Shinyanga tangu Machi 4, 2026 kwa ziara ya siku nne akifuatilia uhai wa chama, kukagua miradi ya maendeleo ambayo Serikali imeweka fedha na kusikiliza changamoto za wananchi kabla ya kuelekea mkoani Simiyu.

More Stories
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi
Kihongosi: Msigombane kwa itikadi za vyama
Kihongosi amtaka mkandarasi kuwalipa vibarua stahiki zao