Agnes Alcardo, Timesmajira Online- Shinyanga
KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Kenani Kihongosi, amemtaka Mkandarasi wa Kampuni ya Sihotech Engineering na AMJ Global Multi Contractors, anayetekeleza mradi wa ujenzi wa stendi ya mabasi Katunda, kuwalipa mara moja vibarua wake stahiki zao.
Agizo hilo limekuja baada ya Katibu huyo wa NEC, kupata taarifa za vibarua hao kutolipwa stahiki zao kwa wakati na kwa muda mrefu huku akisisitiza mkandarasi huyo kukamilisha mradi huo kwa wakati.

Kihongosi amesema hayo Machi 6, 2026 alipotembelea mradi wa stendi ya mabasi Katunda, uliogharimu kiasi cha shilingi bilioni 26 zinazojumuisha ujenzi wa barabara kilomita 6 na jengo la utawala la wahandis,wakati alipokuwa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, akiendelea na ziara yake ya kichama mkoani Shinyanga,
Amesema lengo kuu ni kuona mradi huo unakamilika kwa wakati uliopangwa ili kuweza kuleta tija pamoja na vibarua hao kulipwa kwa wakati stahiki zao,ambao hulipwa kiasi cha shilingi 16,050 kwa siku.
, “Mradi huu ukikalimika utakuwa mkombozi kwa wananchi hususani kwa wakazi wa Shinyanga katika masuala ya usafiri na uchumi.Jambo kubwa na zuri ni kuona mradi huu unakamilika kwa wakati,natoa rai kwa mkandarasi kuongeza kasi na vifaa vya ujenzi ili kufikia Oktoba uwe umekamilika,”amesema Kihongosi.

Pia, amesema kuwa, chama hicho kitaendelea kusimamia utekelezaji wa Ilani ya CCM pamoja na kuwakemea watumishi wa Serikali wenye nia ya kukwamisha maendeleo.
Aidha ameupongeza uongozi wa Mkoa wa Shinyanga kwa kusimamia na kutekeleza miradi hiyo, huku akiwaomba wananchi wa Mkoa huo kutunza miundombinu hiyo ili iweze kuleta manufaa kwa wananchi.


More Stories
Kihongosi: Msigombane kwa itikadi za vyama
DC Mbozi afuturisha wananchi, asisitiza mshikamano na Umoja.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali: Nina imani mubna utendaji kazi wa ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria