Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Mbeya
NAIBU Waziri wa Viwand ana Biashara Exaud Kigahe amesema,Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo na vya Katika (SIDO) linatakiwa lijiendeshe kibiashara lifikie hatua ya kujitegemea ili liweze kutoa gawio kwa Serikali badala ya kuendelea kutegemea ruzuku ya serikali kila siku katika uendeshaji wa shughuli zake.
Naibu Waziri Kigahe ametoa kauli hiyo jijini Mbeya alipofanya ziara ya kutembelea ofisi ya SIDO mkoani humo na Viwanda vyake Pamoja na viwanda vya wajasiriamali wanaochakata zao la mpunga.
“Tunataka SIDO lijiendeshe kibiashara ,tunataka tuiuhishe sheria ya kuendesha SIDO ili kulipa shirika hilo ‘mandet’(mamlaka) ya kujiendesha kibiashara badala ya kutegemea ruzuku ya serikali,
“Tunataka SIDO ijitegemee ,ijiendeshe kwa ubora iwahudumie wananchi na itoe gawio kwa serikali.”amesisitiza Kigahe
Aidha ameliagiza Shirika hilo kwa kushirikiana na TIRDO,KAMATEC,TEMDO wahakikishe teknolojia za kuwasadia wananchi hususan wakulima zifike hadi ngazi za halmashauri na kata ili waweze kuwahudumia wananchi na kuwawezesha kuwa na teknolojia za kuchakata mazao hatua itakayowaongezea ari kwenye uzalishaji.
Awali Kaimu Meneja wa SIDO mkoa wa Mbeya Salma Galasi amesema katika kutimiza azma ya Serikali kuifanya Tanzania kuwa na uchumi unaotegemea viwanda ifikapo 2025,SIDO mkoa wa Mbeya limeendelea kutekeleza shughuli mbalimbali ikiwemo kutumia kituo cha uendelezaji Teknolojia katika kutengeneza mashije,vipuri na kukarabati mitambo ili kuchochea uanzoshwaji na uendelezaji viwanda vidogo mjini na vijijini.
“Katika kipindi cha 2016 hadi 2023 kituo kilitengeneza jumla ya mashine 693 ambazo zilitengeneza ajira 2,272 ,pia kituo kilifanikiwa kutengeneza mashine 558 kwa ajili ya kunawia mikono kipindi cha janga la corona.”amesema Galasi
Aidha ametumia nafasi hiyo kueleza changamoto zinazoikabili SIDO Mkoa wa Mbeya kuwa ni Pamoja na upatikanaji wa maeneo ya kuanzisha kongano za viwanda,bado fedha za mfuko wa wajasiriamali wadogo wananchi ni kidogo na hivyo kukosekana ufanisi wa kutoa fedha hizo kwenye maeneo hasa ya vijijini.
More Stories
Gavu aanika miradi iliyotekelezwa na Serikali ya awamu ya sita Geita
RC Makongoro: Samia aungwe mkono nishati safi ya kupikia
TAKUKURU,rafiki yanufaisha wananchi Mwanza