Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online KAMISHNA Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata
amewataka watumishi wa umma pamoja na wadau wa mamlaka hiyo kuhakikisha wanalitumikia taifa kwa uaminifu na kuzingatia maadili ya kitanzania ikiwemo sheria,kanuni na taratibu za kazi.
Kidata ametoa rai hiyo jijini Dar es salaam April 5 , 2024 katika hafla ya Futari pamoja na watumishi na wadau wa Mamlaka wa Mamlaka ya Mapato Tanzania.
Amesema watumishi wa umma hasa wafanyakazi wa TRA wanajukumu la kuhakikisha wanajitahidi kuwa wakweli, waadilifu na wanaowajibika katika kazi zao ili waweze kuleta matokeo chanya katika jamii.
“Ni wazi tunapaswa kuwa mfano bora kwa wengine na kuonesha kuwa kwa pamoja tunaweza kulipa kodi na kukusanya mapato ya Serikali kwa ufanisi na uaminifu mkubwa ili kulijenga Taifa letu,”amesema Kidata.
Amesema kupitia mwezi Mtukufu wa Ramadhan ni wakati mzuri wa kufanya tafakari juu ya matendo ya kila siku kwa kuzingatia wajibu wa kulipa kodi kama wananchi wenye uzalendo na nchi.
Pia amesema TRA itaendelea kushirikiana, kufanya kazi kwa bidii na dhati kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.
Vilevile amesema kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhan ni muhimu kwa jamii nzima ya kiislamu duniani kote kwa kuwa ni wakati wa kukamilisha ibada ya kufunga kama ilivyoamrishwa na Mwenyezi Mungu.
“Mwezi mtukufu wa Ramadhan ni kipindi kinachotuweka karibu na pamoja kwa wingi katika ibada za swala, madarasa ya dini na kufuturu pamoja kama wanafamilia,”amesema Kidata.
Aidha aliwataka jamii nzima ya kiislamu w kuuzingatia mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa kuzindisha ibada na kuimarisha mshikamano.
More Stories
Gridi za Tanzania, Kenya kuimarisha upatikanaji wa umeme
Mama Zainab:Watoto yatima ni jukumu la jamii yote
DC Korogwe awataka viongozi wa vijiji kuwatumikia wananchi kwa uadilifu