November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kichuya sasa ni ruksa, CEO Simba, Namungo wafunguka

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

BAADA ya kuibuka kwa maswali mengi na kuzuka kwa sintofahamu kuwa iweje kiungo wa timu ya Namungo FC, Shiza Kichuya kuitumikia timu yake katika mchezo wa juzi dhidi ya Azam FC ikiwa Shirikisho la Soka Ulimwenguni (FIFA) lilimfungia miezi sita kucheza soka, Afisa Mtendani Mkuu wa klabu ya Simba, Barbara Gonzalez pamoja na uongozi wa Namungo wameibuka na kutolea ufafanuzi jambo hilo.

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) uliochezwa kwenye uwanja wa Azam Complex na kumalizika kwa sare ya bao 2-2, Kichuya aliingia kuchukua nafasi ya Abeid Athuman na kuibua maswali mengi kwa wadau.

Itakumbukwa kuwa, wiki iliyopita FIFA ilitangaza kuipiga faini ya dola za Kimarekani 127,000 ambazo ni zaidi ya milioni 294 klabu ya Simba au kufungiwa kufanya usajili kwa kipindi cha miaka mitatu kutokana na kumsajili kimakosa winga huyo kimakosa.

Barua waliyotumwa na FIFA kwenda kwa klabu ya Namungo ambayo ndiyo anayoitumikia Kichuya iliwataarifu kuwa, hawataruhusiwa kumtumia mchezaji huyo ambaye amefungiwa kwa kipindi cha miezi 6 kucheza soka baada ya kusajiliwa klabu ya Simba akitokea Pharco Fc bila kufuata taratibu za usajili.

Ilielezwa kuwa, Pharco FC iliamua kumshtaki Kichuya FIFA baada ya kuondoka bila kufata taratibu za uhamisho huku akiitumikia bila kuwa na vibali vya kazi (Release letter).

Kufuatia sakata hilo, uongozi wa Namungo kupitia kwa Ofisa Habari wake, Kindamba Namlia ulikiri kupokea barua hiyo kutoka FIFA ikieleza kuwa, mchezaji huyo hataruhusiwa kuwatumikia hadi Simba itakapolipa faini kwa kosa la kumsajili Kichuya huku akiwa na mkataba na timu hiyo ya Misri.

Lakini baada ya mchezo dhidi ya Azam, Namlia aameuambia Mtandao huu kuwa, kwa sasa Kichuya ataendelea kuitumikia timu hiyo kutokana na klabu ya Simba kuomba FIFA kufanya mapitio upya ya shauri linalomhusu Kichuya.

Kutokana na kuomba upya kupitiwa kwa hukumu hiyo kunafanya kila kitu kuanza upya hadi mapitio mengine yatakapotolewa.

Akitoa ufafanuzi wa sakata hilo , Barbara amesema kuwa, wao kama klabu hawakupewa taarifa FIFA wala ufafanuzi wa kesi hiyo na pia barua iliyotolewa ni kama haikuwa wazi hivyo wao kama klabu hawana mashaka yoyote na Kichuya ni mchezaji huru hadii pale FIFA itakapotoa maamuzi.

“Hadi sasa hatujapewa taarifa yoyote hivyo tunasubiri FIFA watoe taarifa rasmi ili pia tuangalie kama tunaweza kukata rufaa, ” amesema Barbara.

Kuhusu usajili ya Kichuya kuja Simba, kiongozi huyo ameweka wazi kuwa, wakati wanamchukua mchezaji huyo walifuata taratibu zote muhimu ikiwemo kupata ITC kutoka klabu hiyo na kupitia Shirikisho la Soka la Misri kuja kwa Shirikisho la Soka hapa nchini (TFF) kwani hakuna mchezaji anayeruhusiwa kucheza nchini akitokea nje hata kama ni mzawa bila ITC yake.

“ITC ya Kichuya ipo na kama watu wanataka kuona kopi zake zipo na kama nilivyoeleza kuwa FIFA wamesem kuwa maamuzi hayo sio ya mwisho kwani si upande wetu wala wa Kichuya uliopowa mlolongo wa hukumu hiyo hivyo hauwezi kuwa na faini yoyote ikiwa haukui unashitakiwa kwa nini,”.

“Pia tumejua kuna mchezo fulani unafanyika na Kichuya ameshapewa taarifa na tunatarajia hivi karibuni ukweli utajitokeza na kujua tunashitakiwa kwa nini na baada hapo tutasoma ili kuona kama tuna kitu cha kujibu,” ameeleza kiongozi huyo.