Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kodi Mtwara, Bi. Maimuna Khatib tarehe 16.12.2024 ameongoza timu ya maofisa wa kodi kutoka TRA Dar es Salaam kuwatembelea walipakodi wa Masasi kwa lengo la kuwashukuru kwa kulipakodi kwa hiyari sambamba na kuwasikiliza changamoto zao kwa lengo la kuzitatua.
Bi. Maimuna amesema hatua hiyo inakuja ikiwa ni katika kutekeleza agizo la Kamishna Mkuu la kuwashukuru na kuwasikiliza walipakodi.
Aidha, Bi Maimuna ametumia nafasi hiyo pia kuwakumbusha walipakodi kufanya malipo ya kodi zao awamu ya nne mapema kabla ya tarehe 31 ya mwezi huu wa Desemba ili kuepusha usumbufu.
More Stories
TRA yawaonya wafanyabiasha wasio waaminifu nchini
NBAA yatangaza matokeo,ufaulu waongezeka
Homera:Viongozi hamasisheni ununuzi wa hatifungani ya miundombinu ya Samia