Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online Mwanza
Mahakama ya Hakimu Mkazi wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza imehairishwa kuanza usikilizwaji wa hoja za awali (PH) katika kesi ya trafiki namba 3675/2023 inayomkabili Mkazi wa Nyasaka wilayani Ilemela mkoani Mwanza, Philipo Mhina (52) kutokana na kukosekana kwa mtandao.
Katika kesi hiyo, Mhina ambaye ni dereva wa gari ya shule ya msingi Nyamuge ya jijini Mwanza anakabiliwa na shtaka la kusababisha kifo cha askari wa usalama barabarani mkoani humo, Sajenti, Stella Alfonce baada ya kuendesha gari hiyo aina ya Mitsubishi yenye namba za usajili T.964 BRJ bila tahadhari na kumgonga askari huyo.
Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Amani Sumari amesema amelazimika kuahirisha shauri hilo hadi Disemba 7, mwaka huu litakapoitwa kwa ajili ya mshtakiwa kusomewa hoja za awali kutokana na mtandao unaotumika mahakamani hapo kutokuwa imara.
“Tunaendesha mashauri haya mtandaoni lakini leo mtandao unasumbua hauko imara, hivyo naahirisha kesi hii hadi Disemba 7, mwaka huu. Mshtakiwa dhamana yako iko wazi kama umekidhi vigezo,” amesema Sumari
Baada ya maelezo hayo, mshtakiwa amekidhi masharti ya dhamana ambayo ni kuwa na wadhamini wawili ambao ni waajiriwa wa Serikali wenye barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa na ameachiwa kwa dhamana.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi