Fresha Kinasa, Timesmajira Online,Musoma
KAYA tano (5) zilizopo Kisiwa cha Rukuba Kata ya Etaro Halmashauri ya Wilaya ya Musoma mkoani Mara hazina makazi baada ya nyumba zao kuzingirwa na maji yaliosababishwa na kuongezeka kwa maji katika Ziwa Victoria hivyo zimepewa hifadhi Kituo cha Afya cha Kisiwani cha Kisiwani humo.
Ambapo waathirika hao wanasema maji yamewafuata kwa takribani mita 30-40 hadi kwenye makazi yao.
Hayo yamebainishwa kupitia taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijni Mei 4, 2024 ambayo imeeleza kuwa kutokana na maji yanaendelea kuongezeka makazi ya kaya nyingine 32 yako hatarini.
Aidha taarifa hiyo imesema kuwa, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo amewasiliana na wataalamu walioko kwenye Ofisi ya Bonde la Ziwa Victoria Mwanza na kupata jibu kuwa maji yameongezeka kwa kiasi cha wastani wa kina cha mita 1.65.
Taarifa hiyo pia imewataka Wananchi wanaoishi karibu na ufukwe wa Ziwa Victoria kulazimika kufuata ushauri watakaopewa na viongozi mbalimbali pamoja na kufuatilia taarifa za utabiri wa hali ya hewa unaotolewa na TMA ili kuepuka mafuriko.
“Ziwa Victoria lenye kawaida ya ujazo wa maji wa takribani kilomita za ujazo 2,424 (cubic kilometres), kwa sasa maji yaongezeka sana. Tuchukue tahadhari kubwa,”meeleza sehemu ya taarifa hiyo.
More Stories
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu