Na Mwandishi wetu,Timesmajira
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa, Cde. Mohammed Ali Kawaida amefika wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza kumfariji, Kheri James ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini aliyefiwa na baba yake mzazi Desemba 03 mwaka huu.

Mwenyekiti Kawaida akiwa nyumbani hapo amesaini kitabu cha maombolezo na kuhani msiba leo tarehe 09 Desemba 2024.
Bwana alitoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Pumzika kwa Amani mzee wetu.


More Stories
Taasisi ya Tulia Trust yamfuta machozi bibi anayeishi kwa kuokota makopo
Askofu Masondole awataka vijana kutofuata mila na desturi zisizokubalika nchini
Dkt.Samia azindua jengo la Makao Makuu ya Mahakama,ataka kasi ya utoaji haki iendane na ubora wa jengo hilo