Na Mwandishi Wetu,Timesmajira
WAKATI Rais Samia Suluhu Hassan akiitaka Mahakama kutenda haki kwa usawa na wakati, watoto wa aliyekuwa Jenerali Tumainieli Kiwelu wanaomba shauri lao la kuondolewa kwa wasimamizi wa mirathi ya baba yao lililofunguliwa May,2024 limalizike.
Rais Samia akiwa kwenye maadhimisho ya wiki ya Sheria nchini amesema Mahakama ni muhimili muhimu wa kutenda haki kwa usawa na wakati huku ikichagiza shughuli za kiuchumi.
Shauri hilo la kuomba kuondolewa kwa wasimamizi wote watatu wa mirathi ya Jenerali Kiwelu lilifingiliwa Mei 21, 2024 na kupewa namba 11987/2024 mbele ya Hakimu Mkazi Eric Rwehumbiza wa Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Walalamikiwa katika shauri hilo ni watoto watoto watatu kati ya tisa wa Jenerali Kiwelu ambao walishindwa kutimiza wajibu wa kuzitambua, kuzikusanya na kuzigawa mali za marehemu baba yao kwa zaidi ya miaka mitatu sasa.
Watoto hao ni Julius, Anita na Robeson Kiwelu wanaodaiwa kushindwa kugawa mali za baba yao kwa watoto wengine sita ambao ni Leslie, Frank, Jimmy, Joyce, Charles na Jeniffer Kiwelu.
Licha ya kukaa kimya muda mrefu, wasimamizi hao wanalalamikiwa kwa kutumia baadhi ya mali bila kiwashirikisha watoto wengine wa marehemu hali inayoongeza hofu ya utapanyaji wa mali hizo kwa faida ya wachache walioaminiwa na Mahakama kupewa usimamizi wa mirathi.
Hata hivyo Desemba 5,2024 Hakimu Rwehumbiza alisoma uamuzi wa Mahakama na kuahidi kutoa ufafanuzi wa uamuzi huo na nakala ifikapo Februari 06,2025.
Jenerali Kiwelu alifariki Dunia Mei 18,2021 ambapo kabla ya kifo chake aliihudumia nchi hii katika nyadhifa mbalimbali ndani na nje ya jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) akishika nafasi za ukuu wa mikoa mitano tofauti.
More Stories
Waumini Kanisa la Kilutheri Afrika Mashariki wamlilia Rais Dkt.Samia
Waumini K.K.A.M watoa kilio chao kwa Rais Samia
PPAA yazuia zabuni zenye thamani ya bilioni 583