Na David John, TimesMajira Online
WAJUMBE wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa wamemchagua Dkt Hussein Mwinyi kuwa mgombea Urais Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika uchaguzi unatarajia kufanyika Oktoba mwaka huu.
Dkt.Mwinyi ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi amechaguliwa kwa Kura 129 sawa na asilimia 78.65%, katika mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete wa White House Makao Makuu ya nchi Dodoma.
Mkutano huo ambao uliongozwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli na Makamu Mwenyekiti Zanzibari na Rais wa Serikali ya Mapinduzi, Dkt Mohamed Shein, Makamu Mwenyekiti Bara, Philip Mangula, Katibu Mkuu wa Chama hicho Dkt Bashir Ally na viongozi wengine waandamizi wa CCM .
Baada ya kuchaguliwa Dkt Mwinyi alonga.
Akizungumza mbele ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu Dkt Hussein Mwinyi alianza kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwani kazi hiyo haikuwa rahisi.
“Msionione nimepungua, kazi hii hakuwa rahisi hivyo namshukuru Mungu na ninyi wajumbe wa mkutano mkubwa kwa imani kubwa mlioonyesha kwangu “amesema Mwinyi .
Dkt Mwinyi amebainisha kuwa kura 129 ni kura nyingi sana na kwamba wajumbe wa mkutano mkuu wameonyesha kuwa na imani naye na hakuna shaka kwamba atalitumikia taifa kwa uwezo wake wote.
Amefafanua kuwa atakuwa tayari kushirikiana na wezake wote na kwamba baada ya kumalizika kwa mchakato huo hivi sasa timu ni moja tu na so zaidi ya hapo.
“Nitashirikiana na viongozi wote wakiwamo wale ambao wameingia kwenye tano bora, hadi tatu wote kwa ujumla tutakuwa pamoja,” amesema Dkt Mwinyi
Mteule huyo ambaye anakwenda kupeperusha bendera ya CCM kwa nafasi ya urais Zanzibar aliwaeleza wajumbe hao kuwa amefanya kazi na mitihani mingi lakini mtihani mkubwa ulikuwa ni wakinyang’anyilo hicho na anaamini kazi hiyo itakuwa sio ya peke yake bali ni ya wote.
“Mungu awabariki sana.” Alimaliza Dkt Mwinyi.
More Stories
Bei za mafuta Novemba 2024,zaendelea Kushuka
TARURA yaomba Mkandarasi aitwe
Ilemela yakusanya bilioni 3.7.robo ya kwanza