Na David John Timesmajira online
KATIBU Mkuu Wizara ya Fedha Dkt.Natu Mwamba amesema kuwa mkutano mkuu wa wakuu wa nchi za Afrika unaojumuisha viongozi wa Serikali na moja ya mambo yatakayozungumzwa ni kuhusu rasilimali watu.
Ambapo pia umelenga vijana na kwamba takwimu zinaonesha kuwa Katika Bara la Afrika kuna zaidi ya watu bilioni 1.2 lakini asilimia 60 ya hao watu ni vijana wenye umri miaka 25.
Amesema kuwa katika mkutano huo vijana watazungumziwa na ili waweze kufanya kazi lazima wawe na afya njema ,stadi za kazi ,elimu lakini kupitia mkutano huo wataona namna rasilimali watu ya vijana lazima ioneshwe katika muktadha halisi.
Dkt.Mwamba amayasema haya leo Julai 24 mwaka 2023 katika kikao chake na waandishi wa habari wakati akizungumzia mwelekeo na maandalizi ya mkutano huo kwa kile ambacho kinakwenda kujadiliwa katika mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika ambao unaaza Julai 25, mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Amefafanua kuwa Afrika imepita katika mambo mengi ikiwemo Uviko-19 na kwa baadhi ya mataifa kulikuwa na kufungiwa ndani ,kulikuwa na upungufu wa huduma za kijamii na shule zilifungwa hivyo wapo waliorudi nyuma kutoka na mazingira hayo yote yanakwenda kuzungumziwa ili kuona mwelekeo wake hususani katika rasilimali watu.
“Maandalizi mpaka sasa hivi yapo vizuri wageni wameaza kufika na leo tumepokea wageni wengi zaidi ambao ni viongozi wakuu wa nchi tumepata uhakika wa uthibitisho wa viongozi wa nchi takribani 30 katika hao kuna Marais ,Makamu wa Rais,Waziri Wakuu na mawaziri ambao viongozi wa msafara na mabalozi pia kuna uthibitisho wa mawaziri 80 .”amesema
Amefafanua kuwa eneo la rasilimali watu inakuwa na sekta tofauti ambapo kuna elimu ,sayansi, afya ,ubunifu ,teknolojia ,ajira na kazi hivyo mawaziri wote kwenye maeneo haya wamethibitisha kuhudhuria kwenye kikao hicho cha wakuu wa nchi.
Pia amesema katika azimio la Dar es Salaam litakalotoka tegemeo lao nikwamba kutakuwa na adhima kabisa ya kupangwa kwamba wanakwenda kuwekeza kwenye rasilimali watu na kuweka sera wezeshi ambazo zitaweza kutoa nafasi za kazi na kutoa tija kwani ili ufanye kazi Kwa tija lazima uwe na afya njema na stadi zitakazokufanya uweze kuajirika na hiyo ndio muktadha mkubwa wa azimio la Dar es Salaam.
Ameongeza kuwa kwa Afrika kuna Kanda nyingi ambapo mwisho kutakuwa na malengo ambayo yatakwenda kupimwa na yataonesha ushindani na UN wanasema ikifika mwaka 2050 kutakuwa na watu bilioni 2.2 na 20100 kutakuwa na watu bilioni 3.2 hivyo hao watu watakao kuwepo karibu asilimia 70 ni vijana hivyo lazima kwenye eneo hilo la vijana liwekezwe sana.
Vilevile amesema kutokana na hali hiyo mataifa ya Afrika yanajikita ili kuweza kuwa kwenye ushindani na kuweza kujiwekeza,kwa upande wa Tanzania kuna uwekezaji mkubwa kwani kuna vituo vya afya ,zahanati,hospitali ambazo zina vifaa vya kutosha,elimu kuazia ya awali hadi sekondari bila malipo hivyo ukiangalia Tanzania iko vizuri.
Amesema kupitia mkutano huo wa wakuu wa nchi za Afrika unaofanyika hapa nchini kuna vivutio vya kila aina lakini pia Kuna muonekano wa taasisi za Jakaya Kikwete, ambazo zitaonesha namna zinavyotoa huduma.
Pia kuna wajasiliamali wadogo kupitia ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam wapo wa kutosha kwa utaratibu walioandaliwa na wataonesha bidhaa walizo nazo ambapo wajasiliamali 100 watakuwepo kwenye viwanja hivyo,hivyo wageni watapata fursa ya kuona vitu vilivyotayarishwa na watatembea maeneo mengine kama Mlimani City ,Kariakoo kote watapita na watakwenda kusimulia kwao baada ya kumalizika kwa mkutano huo.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba