Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Francis Michael ameahidi ushirikiano kwa watumishi katika utendaji ili kutekeleza maono ya Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mambo yalioainishwa katika ilani ya Chama cha Mapinduzi kuhusu Sekta ya elimu.
Dkt. Michael amesema hayo jijini Dodoma alipowasili wizarani hapo na kuzungumza na watumishi ambapo amesema katika mchakato wa mabadiliko ya mitaala inayoendelea jukumu lake litakuwa ni kuhakikisha inajielekeza katika kutatua changamoto ya kukosekana kwa ujuzi kwa baadhi ya kada za kiutumishi
“Ili kuziba pengo lililopo, tutawasiliana na utumishi kujua mahitaji ya ujuzi na kada za kiutumishi zinazohitajika ili mitaala inayobadilishwa ilenge kuziba pengo hilo katika soko la ajira la ndani na nje ya nchi,” amesema Dkt. Michael.
Ameongeza kuwa Serikali sasa inafanya pamoja na kuboresha Sera ina mkakati wa kuimarisha vyuo vya kati vinavyotoa Diploma ili kuziba pengo la ujuzi unaotakiwa katika soko la ajira la ndani na nje ambapo tayari kipitia Mradi HEET vyuo hivyo vitajengwa katika mikoa 15.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa