November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Katibu Mkuu Mahimbali akabidhi uenyekiti wa kamati nchi zinazozalisha Almasi Afrika,Tanzania yaahidi kuendelea kutoa ushirikiano

Na Mwandishi wetu,Timesmajira online

KATIBU Mkuu Wizara ya Madini Kheri Mahimbali amekabidhi rasmi Uenyekiti wa Kamati ya Wataalam wa Nchi Zinazozalisha Almasi Afrika (ADPA) kwa Katibu Mkuu Wizara ya Madini na Maendeleo ya Migodi wa Jamhuri ya Zimbabwe Pfungwa Kunaka katika kikao cha wataalam kilichofanyika Machi 22, 2023 Victoria Falls, nchini Zimbabwe.

Akizungumza katika kikao hicho, Mahimbali amesema kwamba, licha ya kuwepo mafanikio kadhaa, bado sekta ya almasi inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo kubadilika mara kwa mara kwa bei ya almasi, ushindani kutoka kwa almasi inayozalishwa maabara na kuendelea kwa tishio la uchimbaji haramu wa madini na magendo na kueleza kuwa, anayo imani kuwa chini ya uongozi wa mrithi wa nafasi hiyo, umoja huo ataendelea kuondokana na vikwazo na hivyo kustawi.

”Hatuna budi kuendelea kuimarisha uhusiano wetu na washirika wetu wa kimataifa, kuongeza uwazi na uwajibikaji, na kutekeleza hatua za kupambana na biashara haramu ya almasi na kuboresha maisha ya wachimbaji wetu na familia zao” amesisitiza Mahimbali.

Akizungumzia nafasi ya Tanzania kama mwenyekiti anayemaliza muda wake amesema kuwa, imekuwa heshima kubwa kwa Tanzania kushika nafasi hiyo na wakati ikimaliza muda wake yapo mafanikio kadhaa yaliyofikiwa na kueleza kuwa endapo yatadumishwa, yatauweka umoja huo katika sehemu nzuri kwenye sekta ya almasi duniani.

Ameongeza kuwa, katika kipindi hicho Tanzania ikiwa mwenyekiti kwa ushirikiano wa nchi wanachama, iliwezesha mchakato wa mageuzi ambao umewezesha kufanyika kwa marekebisho ya Katiba ya umoja huo na Kanuni za Ndani za Sekretarieti ya Utendaji ya ADPA ambazo zimewezesha kuajiri rasilimali watu na kufanya uteuzi wa maafisa wanaofaa ambao watasimamia umoja huo kwa kipindi cha miaka minne ijayo baada ya mikutano kadhaa ya mchakato wa kuwapata maafisa hao.

Pia, ametumia fursa hiyo kuwashukuru nchi wanachama wote kwa kuunga mkono na kujitolea katika dhamira ya kuuimarisha umoja wa ADPA na kueleza kuwa, bidii na kujitolea, shauku ya wanachama na Sekretarieti imekuwa chachu ya mafanikio ya umoja huo ambayo kwa njia tofauti imepelekea kuwepo kwa mabadiliko katika maisha ya mamilioni kote Afrika.

Kwa kutambua mchango wa mtangulizi wake Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Adolf Ndunguru,7 aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Mahimbali amemshukuru kwa kuongoza Kamati ya wataalam wa ADPA katika kipindi ambacho Tanzania imekuwa mwenyekiti na kueleza,’’ wakati Tanzania ikiachia madaraka kwenye nafasi ya uenyekiti, natarajia kuendelea kuunga mkono umoja huu na kazi yake muhimu. Nina hakika kwamba mustakabali wetu utakuwa thabiti, na ninawatakia kila la heri katika majadiliano ya leo juu ya ajenda zilizo mbele yetu”.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Madini na Maendeleo ya Migodi Zimbabwe Pfungwa Kunaka akipokea uenyekiti amesema amefurahishwa na hotuba ya Katibu Mkuu Mahimbali na kuahidi kuendeleza pale Tanzania ilipoishia.

“Tutaendelea kuwa wamoja ili kufanikiwa katika umoja wetu. Tunaendelea kutambua uhusiano wetu kupitia Mawaziri wetu kwa kuendelea kufuata miongozo ya Serikali zetu,’’ amesema.

Baada ya kikao cha wataalam, kitafuatiwa na kikao cha Baraza la Mawaziri Machi 23, 2023 ambapo taarifa mbalimbali zitajadiliwa na kutolewa maamuzi.

ADPA inajumuisha nchi 18 ambapo kati yake 12 ni wanachama wanaozalisha almasi na sita ni waangalizi ambao nchi zao kijiolojia zina uwezo wa kuzalisha almasi na mwisho zinaweza kuwa wazalishaji wa almasi siku za karibuni.

Nchi wanachama wanaounda umoja huo ni Angola, Botswana, Cameroon, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Ghana, Guinea, Namibia, Sierra Leone, Afrika Kusini, Tanzania, Togo na Zimbabwe na nchi waangalizi ni Algeria, Jamhuri ya Kongo (Brazaville), Gabon, Ivory Coast, Liberia, Mali na Mauritania. kilichofanyika Machi 22, 2023 Victoria Falls, nchini Zimbabwe.

Akizungumza katika kikao hicho, Mahimbali amesema kwamba, licha ya kuwepo mafanikio kadhaa, bado sekta ya almasi inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo kubadilika mara kwa mara kwa bei ya almasi, ushindani kutoka kwa almasi inayozalishwa maabara na kuendelea kwa tishio la uchimbaji haramu wa madini na magendo na kueleza kuwa, anayo imani kuwa chini ya uongozi wa mrithi wa nafasi hiyo, umoja huo ataendelea kuondokana na vikwazo na hivyo kustawi.

”Hatuna budi kuendelea kuimarisha uhusiano wetu na washirika wetu wa kimataifa, kuongeza uwazi na uwajibikaji, na kutekeleza hatua za kupambana na biashara haramu ya almasi na kuboresha maisha ya wachimbaji wetu na familia zao” amesisitiza Mahimbali.

Akizungumzia nafasi ya Tanzania kama mwenyekiti anayemaliza muda wake amesema kuwa, imekuwa heshima kubwa kwa Tanzania kushika nafasi hiyo na wakati ikimaliza muda wake yapo mafanikio kadhaa yaliyofikiwa na kueleza kuwa endapo yatadumishwa, yatauweka umoja huo katika sehemu nzuri kwenye sekta ya almasi duniani.

Ameongeza kuwa, katika kipindi hicho Tanzania ikiwa mwenyekiti kwa ushirikiano wa nchi wanachama, iliwezesha mchakato wa mageuzi ambao umewezesha kufanyika kwa marekebisho ya Katiba ya umoja huo na Kanuni za Ndani za Sekretarieti ya Utendaji ya ADPA ambazo zimewezesha kuajiri rasilimali watu na kufanya uteuzi wa maafisa wanaofaa ambao watasimamia umoja huo kwa kipindi cha miaka minne ijayo baada ya mikutano kadhaa ya mchakato wa kuwapata maafisa hao.

Pia, ametumia fursa hiyo kuwashukuru nchi wanachama wote kwa kuunga mkono na kujitolea katika dhamira ya kuuimarisha umoja wa ADPA na kueleza kuwa, bidii na kujitolea, shauku ya wanachama na Sekretarieti imekuwa chachu ya mafanikio ya umoja huo ambayo kwa njia tofauti imepelekea kuwepo kwa mabadiliko katika maisha ya mamilioni kote Afrika.

Kwa kutambua mchango wa mtangulizi wake Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Adolf Ndunguru, aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Mahimbali amemshukuru kwa kuongoza Kamati ya wataalam wa ADPA katika kipindi ambacho Tanzania imekuwa mwenyekiti na kueleza,’’ wakati Tanzania ikiachia madaraka kwenye nafasi ya uenyekiti, natarajia kuendelea kuunga mkono umoja huu na kazi yake muhimu. Nina hakika kwamba mustakabali wetu utakuwa thabiti, na ninawatakia kila la heri katika majadiliano ya leo juu ya ajenda zilizo mbele yetu”.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Madini na Maendeleo ya Migodi Zimbabwe Pfungwa Kunaka akipokea uenyekiti amesema amefurahishwa na hotuba ya Katibu Mkuu Mahimbali na kuahidi kuendeleza pale Tanzania ilipoishia.

“Tutaendelea kuwa wamoja ili kufanikiwa katika umoja wetu. Tunaendelea kutambua uhusiano wetu kupitia Mawaziri wetu kwa kuendelea kufuata miongozo ya Serikali zetu,’’ amesema.

Baada ya kikao cha wataalam, kitafuatiwa na kikao cha Baraza la Mawaziri Machi 23, 2023 ambapo taarifa mbalimbali zitajadiliwa na kutolewa maamuzi.

ADPA inajumuisha nchi 18 ambapo kati yake 12 ni wanachama wanaozalisha almasi na sita ni waangalizi ambao nchi zao kijiolojia zina uwezo wa kuzalisha almasi na mwisho zinaweza kuwa wazalishaji wa almasi siku za karibuni.

Nchi wanachama wanaounda umoja huo ni Angola, Botswana, Cameroon, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Ghana, Guinea, Namibia, Sierra Leone, Afrika Kusini, Tanzania, Togo na Zimbabwe na nchi waangalizi ni Algeria, Jamhuri ya Kongo (Brazaville), Gabon, Ivory Coast, Liberia, Mali na Mauritania.