Na Mwandishi wetu Timesmajira online Dar es Salaam
MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Kate Kamba anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Vijana (CCM) Kata ya Mabibo ambao unatarajia kufanyika Desemba 30, mwaka huu katika ukumbi wa Chuo cha Usafirishaji Taifa (NIT).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari imeeleza kuwa Mkutano huo umelenga kwenda kufanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo sambamba na kuyaelezea yale yote mazuri yaliofanywa katika utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Imeeleza kuwa mkutano huo utakwenda sambamba na kampeni ya duka la mama Lina bidhaa nzuri njoo ujionee, ambapo wauza duka wa bidhaa hizo ni viongozi mbalimbali kutoka Chama cha Mapinduzi CCM ambao ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu, Mbunge, Diwani pamoja na wenyeviti wa Serikali za mitaa.
“UVCCM Mabibo imekuaja na kampeni ya kulitangaza duka lenye bidhaa nzuri na makini kabisa ambapo wauza duka wao ni makini ambayo ni miradi ya maendeleo” imeeleza
Miongoni mwa bidhaa hizo, ni Barabara (Lami) NIT-Mburahati -Magomeni, Matundu ya vyoo shule ya msingi Mabibo,wadi ya wazazi zahanati ya Mabibo, ukarabati barabara ya Lami Mabibo- Big Brother, Madarasa 8 ya Sekondari Mabibo pamoja Uzio shule ya Msingi Mpakani.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa Mkutano huo umebeba kauli mbiu “Tupo sambamba na wauza duka wetu”, kwani bidhaa za mama zinauzika”
Aidha , Wananchi wametakiwa kujitokeza katika Mkutano huo ili kujionea bidhaa hizo.
More Stories
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake