Na Judith Ferdinand, TimesMajira Online, Mwanza
WANANCHI wa Kata ya Ilemela wameahidiwa neema katika sekta ya afya endapo watachagua viongozi wanaotokana na Chama cha Mapinduzi(CCM) kwa nafasi ya Urais, Ubunge na Udiwani katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 28 mwaka huu.
Ahadi hiyo imetolewa na mgombea Ubunge Jimbo la Ilemela kupitia CCM, Dkt. Angeline Mabula wakati akizungumza na wananchi wa Kata hiyo kwenye mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Ilemela.
Amesema, endapo watashinda atajenga zahanati hiyo pamoja na kuboresha kituo cha Afya cha Lumala ambapo tayari Serikali imetenga milioni 60 kwa ajili ya maboresho hayo ili kuhakisha huduma ya mama na mtoto inapatikana kwa urahisi.
Mbali na zahanati pia amesema, milioni 44 zimetengwa kwajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo 10 katika shule ya sekondari Lumala pamoja na shule ya msingi Mwambani huku Halmashauri ikitenga milioni 151 kwa ajili ya ujenzi wa barabara za Ilemela-Mahakamani, Majengo mapya-Lumala, Pasiansi-Kiseke.
Kwa upande wake, mgombea udiwani wa Kata ya Ilemela kupitia CCM, Wilbard Kilenzi amesema, katika hiyo jumla ya viwanja 1260 vimepimwa na Serikali ilitoa bilioni 3.30 kwajili ya kumaliza mgogoro wa ardhi katika eneo la Nyakuguru huku Serikali ikifanikisha kutatatua mgogoro wa makaburi baina ya wakristo na waislamu katika eneo la Lumala.
“Mbali na hayo kwa juhudi za Dkt.Angeline, mimi, wananchi na Serikali tumefanikiwa kujenga madarasa matatu katika shule ya msingi Jeshini na Mwambani pamoja na darasa moja katika shule ya msingi Sabasaba,hivyo nawaomba mtu chague ili tukafanye maendeleo zaidi,” amesema Kilenzi.
Meneja Kampeni wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Jimbo la Ilemela Kazungu Idebe, amewaambia wanailemela kuwa wanayosababu milioni 100 ya kumchagua Dkt. John Magufuli na wagombea wanaotokana na chama hicho.
Idebe amesema, kwa kipindi cha miaka mitano katika sekta ya afya zahanati zaidi ya 1000 zimejengwa,vituo vya afya zaidi ya 400 na hospitali za Wilaya zaidi ya 90 ikiwemo ya Wilaya ya Ilemela.
Amesema, katika kipindi hicho pia kwa Jimbo la Ilemela wamefanikiwa kujenga shule za msingi mpya tatu,sekondari tatu na mbili za kidato cha tano na sita,barabara zimejengwa.
More Stories
Wananchi Kiteto waishukuru Serikali,ujenzi wa miundombinu ya barabara
Watoto 61 wenye mahitaji maalum washikwa mkono
Mtoto wa mwaka mmoja na miezi kumi,adaiwa kubakwa na baba wa kambo