Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala
KAMATI ya Maendeleo ya Kata ya Ilala imebadilisha jina la Shule ya Sekondari Kusuru iliyopo Ilala kwa sasa Shule hiyo itaitwa Mussa Zungu Sekondari .
Kamati hiyo ya Maendeleo ya Kata imebadilisha jina hilo kwa heshima ya Mbunge wao Mussa Zungu ambaye ndio Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akizungumza katika kikao hicho cha Maendeleo ya Kata kilichowashirikisha Wadau wa Maendeleo ,Watendaji wa Serikali ,Walimu ,na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Diwani wa Kata ya Ilala Saady Khimji alisema pia mtaa wa Mafuriko kwa sasa Kamati ya Maendeleo wamekubaliana rasmi utaitwa Mtaa wa Bungoni .
“Katika kikao chetu cha kujadili Maendeleo tumeweza kujadili mambo mbalimbali ikiwemo sekta ya Elimu Barabara ,afya na kuwasilisha vipaumbele vya kutengeza Barabara kwa mwaka wa fedha 2023/2024 ” alisema Khimji .
Diwani Kimji alisema kwa sasa Kata ya Ilala INATARAJIA kuwa ya kisasa katika utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi ambayo inaongozwa na RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
Mwenyekiti wa chama Cha Mapinduzi CCM Habib Nasser alitoa kero ya soko la Ilala Boma ambalo lilikuwa KUTOA huduma mwisho saa nne kwa Sasa soko hilo linatoa huduma massa 24 kupelekea kero wakazi wa eneo hilo wanashindwa kufanya huduma za Jamii ikiwemo misiba ikitokea lazima wamie Mtaa wa pili hivyo wameishauri Halmashauri kutazama upya suala hilo .
Mwenyekiti Habib alisema kuhusu changamoto zingine zilizopo Ilala watazitatua kwa kushirikiana na Ofisi ya Diwani wa Kata ya Ilala Saady Khimji na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu .
Diwani wa Viti Maalum Wanawake Wilaya ya Ilala Aisha Kipini aliwataka Wazazi kutenga muda kuzungumza na watoto wao wawe marafiki Kila wakati kwa ajili ya kukabiliana na vitendo vya ukatili .
Aidha Diwani Aisha alipiga MARUFUKU wazazi kutuma watoto sokoni na dukani nyakati za usiku kwani ukimwengu umebadilika watu wanawafanya vitendo Vya ukatili watoto .
Diwani wa Viti Maalum Wanawake Ilala Mwalimu Beatrice Edward amewataka Walimu na Wazazi kwa kushirikiana na uongozi wa Kata ya Ilala washirikiane Ili kutokomeza ZIRO kwa Wanafunzi .
More Stories
RC Chalamila awataka ndugu,Jamaa na marafiki kuwa wavumilivu zoezi la uokoaji likiendelea
Baraza la Madiwani lafukuza watumishi wawili idara ya afya
Wanasheria waombwa kusaidia kusimamia sheria, sera ulinzi wa taarifa