February 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kasulu FC mabingwa mashindano Khimji 2025

Na Heri Shaaban,Timesmajira Online,Ilala

TIMU ya Kasulu FC ya Kata ya Ilala,mabingwa mashindano ya mpira miguu wa kombe la Khimji (Khimji Super CUP) 2025,yalioshirikisha timu zaidi ya 20.

Kasulu FC,waneibuka na ubingwa huo katika fainali ya mashindano hayo yaliofanyika uwanja Garden Ilala ,baada kuifunga timu ya Searose FC goli 4-1,hivyo kujinyakulia ambapo Kasulu fc wamejinyakulia kitita cha milioni 1,seti ya jezi, medali 22 na mpira

Akizungumza katika fainali hiyo Mratibu wa mashindano hayo,Diwani wa Kata ya Ilala,Saady Khimji,amesema mshindi wa pili wa mashindano hayo timu ya Searose FC,imejinyakulia kiasi cha 500,000, seti moja ya jezi, medali na mpira mmoja.

Pia amesema,mashindano mengine yanatarajia kuanza mwezi huu ya kutafuta kombe la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt samia suluhu Hassan, yatakayojulikana Samia Super Cup 2025 .

“Dhumuni ni kukuza vipaji kwa vijana,kwani michezo ni ajira,afya,ujenga uhusiano hivyo timu hizi za mchangani zina uwezo wa kutoa wachezaji wa ligi kuu mpaka wa kimataifa,”amesema Khimji.

Kada wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ilala Selemani Kaniki, katika michezo hiyo alitoa shilingi 200,000,ambazo walipatiwa mchezaji bora shilingi 100,000 na golikipa bora shilingi 100,000.