January 24, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kassim Mganga kuwasha moto siku ya wapendanao

Na jackline Martin TimesMajira Online

Siku ya wapendanao jumapili ya 12. Februari watu mbalimbali wanakaribishwa kusherehekea upendo huo na sauti za Kassim Mganga na Nguza Viking katika tamasha la ‘Dance away Valentine’

Hafla hii itaashiria onyesho lake la kwanza jukwaani na itampa nguza Viking mwanamuziki mashuhuri fursa na heshima anayoistahiki ya kuanzia tena kazi zake za muziki.

Kassmim Mganga ambaye ni mwanamuziki wa kizazi cha pili na Nguza Viking ambaye ni msanii wa kizazi cha kwanza wamejumuisha juhudi na ubunifu wao wa kutengeneza muziki mpya ambao ulizinduliwa hivi karibuni ambao ni ‘Harusi yangu’ na ‘Zafarani’

Wanguli hawa watasaidiwa na msanii Banana zorro na bendi yake ya the B Band pia watasindikizwa na wasanii wa kizazi kipya Neddy Music na Nally ambao watatumbuiza kama onyesho la ufunguzi kwenye hafla hii itakayoendeshwa na MC mashuhuri Taji Liundi .

Tamasha la Dance Away Valentine litafanyika katika hoteli ya Sea Cliff huko Masaki Jumapili tarehe 14 Februari kuanzia saa moja jioni na kuendelea .

Hafla hiyo iko wazi kwa umma na watu wanahimizwa kuja kuunga mkono wasanii legendary wa muziki nchini Tanzania kwani wahenga wanasema ‘kale ni dhahabu’