Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
RAISI wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk, Hussein Ali Mwinyi amewahimiza Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Kuchangamkia Fursa za Kiuchumi zitakazokuwepo kwenye Miradi mikubwa ya Maendeleo iliyomo Mkoani humo .
Rais Dk, Mwinyi ametoa Tamko hilo alipoweka Jiwe la Msingi Mradi wa Nyumba 370 za Maakazi na Biashara ziliopo Mangapwani Wilaya ya Kaskazini B, Mkoa wa Kaskazini Unguja Ikiwa ni Nyumba za Fidia kwa Wananchi walioathirika na Ujenzi wa Barabara katika Eneo la Mangapwani ikiwa ni sehemu ya Ujenzi wa Bandari Jumuishi ya Mangapwani.
Dk, Mwinyi ameeleza kuwa Miradi inayoendelea katika Mkoa huo italeta Mabadiliko makubwa ya Maendeleo na Kiuchumi yanayopaswa kuchangamkiwa na Wanachi Kuondokana na Umasikini.
Ameuelezea Mradi wa Bandari Shirikishi ya Mangapwani na Ujenzi wa Barabara kuwa ni miradi itakayowaleta Wafanyakazi wengi wa Kigeni watakaohitaji Nyumba za Makaazi na Huduma mbalimbali za Kijamii ni fursa kwa Wananchi.
Rais Dk, Mwinyi amefahamisha kuwa hiyo ni fursa muhimu kwa Wananchi Kuinuka Kiuchumi na Maendeleo ya Kijamii.
Akizungumzia Suala la Fidia kwa Wananchi Rais Dk,Mwinyi ametoa Agizo la Kila Mwananchi Kulipwa kile anachotaka ikiwa Malipo ya Fedha au Nyumba.
“Kila Mwanachi atalipwa kwa kile anachotaka wa fedha alipwe fedha na anaetaka Nyumba atalipwa nyumba” amesisitiza Dk, Mwinyi
Amewahakikishia Wananchi kuwa Serikali Itamlipa kila Mwananchi haki yake na hakuna Mwananchi atakae sononeka kwa Kukosa Fidia.
Akizungungumzia Ujenzi wa Bandari ya Mangapwani ameeleza kuwa tayari Mkandaarasi tayari amelipwa Malipo ya Awali na ameanza kazi za Upinaji wa sampuli za Udongo katika Eneo hilo kuelekea kuanza Ujenzi.
Aidha ameeleza kuwa Serikali inakusudia kujenga Uwanja Mkubwa wa Michezo( Football Academy) katika Mkoa wa Kaskazini Unguja utakaokuwa na Viwango vya Kisasa.
Aidha amefahamisha kuwa Serikali imepanga kuvifanyia Ukarabati Mkubwa Viwanja Vya Gombani Kisiwani Pemba , na Mao Tse Tung na kukamilisha Ujenzi wa Viwanja vya Maisara Sports Complex baadae kujenga Academy hiyo Kaskazini Unguja.
Rais Dk Mwinyi ametoa pongezi kwa Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi ,Wakala wa Majengo ZBA kwa Usimamizi mzuri uliofanikisha Ujenzi wa Nyumba hizo pamoja na Mkandarasi wa Ujenzi huo Kampuni ya ORKUN ya Uturuki.
Naye Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuz Dk, Khalid Salum Muhammed amewakikishia Wanachi kuwa Barabara Zote zinazojengwa hivi sasa hapa nchini zinajengwa kwa Viwango vya Kimataifa vya Ubora.
Aidha ameeleza kuwa Serikali tayari imeingia Makubaliano na Kampuni ya ORKUN GROUP ya Ujenzi wa Barabara ya Kilomita 8 ya Mfenesini hadi Bumbwini na Barabara ya Mahonda -Zingwezingwe hadi Pangatupu kiwango cha lami.
Akiwasilisha Taarifa ya Kitaalamu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Dk, Habiba Hassan amefahamisha kuwa Ujenzi wa Nyumba hizo 370 katika eneo la hekta 30 utaambatana na Ujenzi wa Barabara za ndani,Mifumo ya maji safi na taka na Mifumo ya kuhifadhi Taka,Msikiti na Eneo la Biashara tayari umefikia asilimia 50 na Malipo ya Mkandarasi yamefikia Dola Milioni 13 na laki Mbili sawa na asilimia 47.91 ya gharama zote za Mradi.
More Stories
Maono ya Rais Samia yanavyozidi kuipaisha Tanzania kupitia utalii
Maofisa Watendaji watakiwa kufanya kazi kwa weledi
Muhoji Sekondari kumaliza changamoto ya umbali kwa wanafunzi Musoma vijijini