November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kasi ukuaji uhusiano Tanzania na China, Dkt.Samia anastahili pongezi

Na Mwandishi wetu.

Tunapoelekea kufunga mwaka 2022, ubalozi unatoa shukrani za dhati kwa wadau mbalimbali kwa ushirikiano wao uliowezesha utekelezaji wa Majukumu ya Ubalozi. Katika Mwaka 2022 mambo mbalimbali yenye tija na manufaa kwa wananchi yamefanyika kufuatia mwongozo na maelekezo ya Mwanadiplomasia No 1 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk Samia Suluhu Hassan miongoni mwa Mambo hayo ni yapo Mambo 14 aliyoyafanya akiwa Ziara ya Kihistoria ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan-nchini China mnamo Novemba 2-4 Novemba 2022 kupitia ziara hiyo Tanzania na China zilipandisha hadhi ya mahusiano kuwa ya Kimkakati katika nyanja zote.

***Mbili
Kwa upande wa biashara, Mauzo ya bidhaa za Tanzania katika soko la China yaliongezeka kutoka Dola za Kimarekani Milioni 409 hadi kufikia Dola za Kimarekani Milioni 605.5. Inatarajiwa katika mwaka 2023 mauzo yataongezeka kwa asilimia 20 kutokana na Tanzania kufunguliwa soko jipya la bidhaa wakati wa ziarw ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan nchini China;

***Tatu
Wakulima na wafanyabiashara wa Tanzania wanaoshughulika na zao la Parachichi walifunguliwa soko jipya la China Mwezi Novemba 2022. Kuanzia msimo ujao wa 2023 mauzo ya parachichi katika soko la China yataanza.

***Nne
Wavuvi wa Tanzania walifunguliwa soko Jipya la kuuza mabondo ya Samaki na samaki aina sangara nchini China Mwezi Novemba 2022. Inatarajiwa mwaka 2023 mauzo ya bidhaa za uvuvi yataongezeka.

***Tano
Bidhaa za Tanzania zilizoongezewa thamani zilianza kuuzwa katika soko la China kupitia Mtandao Maarufu wa Biashara wa JD.COM wenye watumiaji milioni 600- Mei 2022.

***Sita
Watanzania walianza kufanya shughuli za usafirishaji wa mizigo yao moja kwa moja kutoka Tanzania hadi China kwa kutumia Shirika la Ndege la Air Tanzania- Mei 2022. Inatarajiwa mwaka 2023 baada ya China kufunguka shughuli zitaongezeka.

***Nane
Kufuatia maelekezo ya Mhe Rais @SuluhuSamia Ubalozi Mdogo wa Tanzania katika jijini la Biashara la China- Guangzhou ulifunguliwa rasmi mwezi Mei 2022. Watanzania wameanza kupata huduma mbalimbali za kufanikisha shughuli zao za biashara na Ubalozi mdogo umeanza kufungua fursa mpya za masoko ya bidhaa.

***Tisa
Filamu ya Tanzania Royal Tour ilioneshwa katika Televisheni ya Hainan Mwezi Oktoba 2022 na kutizamwa na watu milioni 60. Aidha filamu hiyo iliyotafsiriwa kwa lugha ya kichina imeoneshwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii ya China.

***Kumi
Wanafunzi wa kitanzania watanufaika kwa kupata shahada na stashahada kufuatia kusainiwa kwa Makubaliano Mwezi December 2022 kati ya Tasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), na Taasisi ya Chongqing Vocation Institute of Engineering (CQVIE) ya China ya kuendesha mafunzo ya pamoja.

***Kumi na Moja
Vijana wa kitanzania wataanza kunufaika na mafunzo ya ufundi kufuatia hatua ya ufunguzi rasmi wa Chuo cha Ufundi cha VETA mkoani Kagera kilichojengwa kwa msaada kutoka China na kuzinduliwa rasmi na Rais Dk.Samia Mwezi Oktoba 2022

***Kumi na Mbili
Watanzania 122 wamepata ufadhili (scholarships) wa masomo ya Elimu ya Juu katika Vyuo Vikuu nchini China katika fani mbalimbali. Mwaka 2023 watanzania wataendelea kupata fursa za masomo ikiwa ni sehemu ya matokeo ya ziara ya Rais Samia nchini China.

***Kumi na Tatu
Katika mwaka 2022 Wafanyabiashara wa Tanzania wamepatiwa elimu kwa umma kuhusu fursa za biashara zilizopo nchini China pamoja na ushauri juu ya hatua za kuchukua ili kuepuka kuangukia mikononi mwa wafanyabiashara wasio waaminifu.

***Kumi na Nne
Katika Mwaka 2022 Vipindi vya Elimu kwa Umma vilianzishwa ili kuwapa wananchi ufahamu juu ya fursa za upatikanaji wa teknolojia mbalimbali za bei nafuu kwa ajili ya uzalishaji/usindikaji wa malighafi zinazopatikana nchini.