Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online, Iringa

MKUU wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela anatarajia kutangaza nia ya kugombea ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) atakapokutana na waandishi wa habari Julai 7.
Kasesela ameuambia Mtandao wa Timesmajira kuwa, lengo lake la kutaka kujitosa katika kinyan’ganyiro cha kuwania Ubunge linatokana na kile alichoeleza kuwa ni kazi zilizofanywa na serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais Dkt John Magufuli.
“Kumekuwa na taarifa zinasambaa za mimi kugombea Kawe lakini Julai 7 ndio siku pekee ya kueleza ukweli juu ya jambo hili katika mkutano wangu na vyombo vya habari utakaofanyika katika ukumbi wa mkutano wa Boma,” amesema Kasesela.
Amesema, hiyo ni siku pekee ambayo ndiyo hasa atategua kitendawili cha wapi atagombea ubunge na kuzima tetesi zilizopo sasa kuwa atagombe jimbo la Kawe, Rungwe au Iringa Mjini.
More Stories
Dkt.Mabula aomba mabonde Ilemela yatumike kwa Kilimo cha umwagiliaji
Ubovu wa barabara mlima Kilimanjaro, changamoto watalii kufikia vivutio vya utalii
Rais Samia afuturisha Makao ya watoto Kikombo