Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
RAIS Mstaafu wa Awamu ya Sita (6) wa Zanzibar, Mheshimiwa Amani Abeid Karume, leo Januari 02 2025, amezindua Jengo la Kituo cha Tiba na Kurekebisha Tabia, huko Kidimni, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.

Ufunguzi wa Jengo la Kituo hicho, ambacho kipo chini ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, ni Sehemu ya Shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Katika hafla hiyo Mhe. Karume ametoa Zawadi mbali mbali, zikiwemo za Vitendea-kazi, kwaajili ya vijana waliofanikiwa kuacha matumizi ya dawa za kulevya, vikijumuisha Vifaa vya Gereji, Cherehani, pamoja na Ng’ombe wa Maziwa.

Viongozi mbali mbali wa Jamii, Vyama vya Siasa, Serikali, Dini, na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, wamehudhuria hapo, wakiongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Mhe. Harusi Said Suleiman; katika Hafla ambayo imetanguliwa na harakati za Burudani zikiwemo Utenzi, Ngoma ya Warowaro na Msondo kutokea Makunduchi, Mkoa wa Kusini Unguja.

More Stories
Mume adaiwa kuua mke kikatili
Mhandisi Mramba:Umeme wa Jotoardhi kuunganishwa kwenye gridi ya Taifa ifikapo 2030
Watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali watakiwa kuendelea kuzingatia maadili ya utumishi wa umma