Na Mwandishi Wetu,
Aliyekuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Muadhama Polycarp Kardinali Pengo leo Machi 16, 2023 amezuru kaburi la aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano HAYATI Dkt. John Pombe Joseph Magufuli nyumbani kwa marehemu kijijini Chato, mkoani Geita. Kardinali Pengo, aliyeongozana na Askofu wa Jimbo Katoliki Geita, Dkt. Flavian Kassala na viongozi wengine wa dini wa Geita, alipokelewa na mjane wa Marehemu Mama Janeth Magufuli na wanafamilia.



More Stories
Mke wa Rais wa Finland atembelea Makumbusho ya Taifa
Lulida ataka viwanda vilivyofungwa vifufuliwe
WMA yahakiki vipimo asilimia 99 ya lengo