Na Ashura Jumapili, TimesMajira Online, Bukoba.
Nazir Karamagi ,amerejea kwenye ulingo wa siasa kwa kishindo baada ya kupata kura 669 na kumbwaga aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Kagera ,Costancia Buhiye aliyedumu katika nafasi hiyo kwa muda wa miaka (15 ) mfululizo aliyepata kura 452.
Awali akitangaza matokeo msimamizi wa uchaguzi huo ambaye ni spika wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk.Tulia Ackson alisema ,atakaye tangazwa kushinda katika uchaguzi huo ndiye kiongozi wa wana ccm wote wa mkoa wa Kagera.
“Mnatakiwa kumheshimu wote ndiye kiongozi wenu hata kama hukumpigia kura na wagombea walioshinda haimanishi kuwa wao ni bora kuliko wenzao bali chama kimeona wote wanafaa kuongoza na CCM ni moja”alisema Dk.Ackson.
Dk.Tulia ,alimtangaza aliyechaguliwa kuwa mwenyekiti wa ccm Mkoa wa Kagera ni Nazir Karamagi aliyepata kura 669,akifuatiwa na Costancia Buhiye aliyekuwa anatetea kiti chake kwa kupata kura 452 ,Novatus Nkwama kura 05 na Mshobozi Medard alipata kura 18.
Pia alimtangaza mjumbe wa halmashauri kuu ccm Taifa kutokea mkoa wa Kagera kuwa ni Karim Amri,aliyepata kura 751 na kumzidi mpinzani wake Wilbrod Mutabuzi aliyekuwa anatetea kiti chake na kupata kura 368 katika uchaguzi huo.Nazir Karamagi,baada ya kutangazwa kuwa mwenyekiti wa Mkoa ,aliwashukuru wajumbe kwa kumuamini ili aweze kuwatumikia.
Karamagi,alisema ofisi yake ipo wazi muda wote kuwasikiliza wanachama wake katika kutatua changamoto mbalimbali na kuleta maendeleo.
Alimuomba mwenyekiti aliyemaliza muda wake Buhiye kumpa ushirikiano katika majukumu yake mapya ya uongozi katika mkoa huo.
Alisema kwa kushirikiana na katibu wa chama hicho mkoa Christopher Paranjo wataanda semina ya uongozi wa viongozi wote wa chama katika mkoa huo ili kuelewa majukumu na wajibu wa vingozi katika chama.
Hata hivyo aliwataka wanachama kuendelea kushikamana na kukijenga chama kwa umoja na kuhakikisha uchaguzi mkuu ujao wa 2025 wanachukua majimbo yote na Kata zote.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa