Na Mwandishi wetu,Timesmajira
SERIKALI imeahidi kutoa ushirikiano mkubwa katika kuwezesha mazingira wezeshi ya biashara ili Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) iweze kukua kwa Kasi na kuwa kimbilio la wafanyabiasha na wawekezaji wa ndani na nje ya Tanzania.
Hayo yamebainishwa mbele ya vyombo vya habari jijini Dar es salaam na Waziri wa Viwanda na Biashara Judith Kapinga baada ya kufanya ziara yake kwenye Mamlaka ya Maendeleo Biashara Tantrade na kubaini taarifa za uwajibikaji kazi amesema ushirikiano ni kitu cha msingi katika uendeshaji wa shughuli mbalimbali za kibiashara.

“Mazingira ya kushirikiano yataleta tija kwa taasisi endapo uendeshwaji wa shughuli mbalimbali utafanywa kwa pamoja na kushirikiana na Taasisi zingine za kiserikali na sekta binafsi kuinua ubora wa kipekee wa huduma zenu katika kuchochea maendeleo ya uchumi na Taifa kwa ujumla,” amesema Kapinga
Aidha Kapinga amesisitiza kwamba bodi ya Tantrade inatakiwa kufanya maboresho ya kiutendaji katika idara mbalimbali Ili iweze kuweka mifumo saidizi ya kikazi ya wao kwa wao kuweza kusomana kwa maendeleo ya taasisi na Serikali kwa ujumla.

Hata hivyo Waziri huyo ameeleza kuwa katika biashara Kuna vikwazo kwamishi vinavyotokana na Sheria zilizokwisha pita muda wake pamoja na kanuni zake viweze kufanyiwa kazi kwa haraka Ili kuweza kuvutia mahitaji ya soko la ndani na nje kwa wafanyabiasha.

More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi