Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
Naibu Waziri Nishati, Judith Kapinga Septemba 17, 2024,ameshuhudia fainali ya mashindano ya kombe la Doto 2024 (Doto Cup 2024),yaliofanyika jimboni Bukombe mkoani Geita.
Mshindi wa kwanza katika fainali hiyo ni timu ya mpira wa miguu,Butinzya huku mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa.
Mashindano hayo yameandaliwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe,Dkt. Doto Biteko.
Mgeni rasmi Innocent Bashungwa,aliikabidhi timu ya Butinzya,ilioibuka kidedea katika mashindano hao,kiasi cha laki tano,seti 3 za jezi na mipira mitatu.
More Stories
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes
Rais Samia: Yanga endeleeni kuipeperusha bendera ya Tanzania
15 wajinoa Juventus,akiwemo mtoto wa Mwenyekiti wa CCM Mbeya