January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kapinga akagua banda la Wizara ya Nishati

Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amekagua banda la Wizara ya Nishati na Taasisi zake,katika tamasha la KIZIMKAZI linaloendelea Visiwani Zanzibar.

Wizara ya Nishati inashiriki katika tamasha hilo kupitia maonesho.Ambapo Wizara inatoa huduma moja kwa moja kwa wananchi kwa kushirikiana na taasisi zake, pamoja na kutoa elimu ya mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kwa mwaka 2024-2034.