Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
MSANII wa hip hop nchini Marekani Kanye West na aliyekuwa mke wake Kim Kardashian, wamekubaliana kumaliza ndoa yao kufuatia tofauti ambazo haziwezi kusuluhishwa. Hivyo wamekubaliana kwamba hakuna kati yao anayehitaji msaada wa mwenzake.
Hata hivyo, Kanye West amekubali kutunza watoto wake wanne kwa ushirikiano na Kim Kardashian. Hatua yake inafuatia ombi la talaka lililowasilishwa na Kardashian Februari 19 mwaka huu, ambalo lilianzisha mchakato wa kumaliza ndoa yao iliyodumu takribani miaka saba.
West na Kardashian wana mabinti wawili – North na Chicago, walio na umri wa miaka saba na mitatu huku wavulana wakiwa wawili. Saint, miaka mitano, na Psalm, anaelekea kuwa na miezi miwili ifikapo mwezi ujao. Kwa mujibu wa ombi la Kardashian, walitenganisha mali zao wakati wote wa ndoa yao kutokana na makubaliano yaliofikiwa kabla ya kuoana.
Wanandoa hao ni miongoni mwa mastaa maarufu zaidi duniani wote wakipata ufanisi mkubwa kivyao. Ndoa yao imekuwa mojawapo ya zinazofuatiliwa kwa karibu katika miongo ya hivi karibuni.
%%%%%%%%%%%%
More Stories
Startimes yazindua makala ya China, Africa
Mwanasheria wa Katavi aliyetimkia kwenye muziki achaguliwa tuzo za MIEMMA
Coca-cola ‘Kitaa Food Fest’ yahitimishwa kwa mafanikio