December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kampuni ya TBL yafanya mkutano wake mkuu wa 51 wa mwaka

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) imefanya mkutano wake mkuu wa 51 wa mwaka ambao umehudhuliwa na wadau mbalimbali na kujadili maendeleo ya TBL na changamoto zinazokabili kampuni hiyo kwa mwaka wa fedha uliopita.

Hayo ameyasema jana Julai 25 2024 Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Bodi ya TBL,Leonard Mususa wakati akizungumza na wanahisa wakati wa mkutano huo ambao uliangazia utendaji wa kifedha wa TBL PLC, mikakati na nafasi yake katika soko.

Amesema ajenda muhimu katika mkutano huo ulikuwa ni udhinishwaji wa gawio la shilingi 537 kwa kila hisa jumla ya shilingi158,445 milioni kwa mwaka uliomalizikaDesemba, 31 mwaka 2023 ni ongezeko la asilimia 85 ikilinganuishwa na mwaka uliopita, hiyo inaonyesha dhamira ya TBL katika kurudisha faida thabiti kwa wanahisa wake.

“Tunajivunia kutangaza kuwa licha ya hali ngumu yam waka 2023 ikijumuisha mvutano wa kisiasa kijografia duniani na ongezeko la ushuru wa ndani TBL PLC inaonyesha ukuaji thabiti na kutoa thamini kubwa kwa wanahisa wetu. Utekelezaji wetu Madhubuti wa mipango ya kimkakati na Imani ya soko katika orodha ya chapa mbalimbali ilisababisha ongezeko kubwa la mapato kutuwezesha kuidhinisha na kusambaza gawio la shilingi 537 kwa kila hisa ongozeko kubwa zaidi la asilimia 85 ilikilinganishwa na mwaka uliopita,” amesema.

Ameongeza kuwa kampuni hiyo inaendelea kutekeleza mkakati wake wa kibiashara ulio thibitishwa na kuongeza mauzo na masoko nyuma ya orodha ya chapa za bi ana zaidi ya bia ili kutoa ukuaji thabiti na kuunda thamani ya muda mrefu na TBL inanunua zaidi ya asilimia 74 ya malighafi zake kutoka ndani ya nchi.

Amesma mwaka 2023 TBL ilipa kodi ya serikali shilingi bilioni586 ikilinganishwa na mwaka uliopita ilikuwa shilingi bilioni 528 kwa mwaka uliopita hivyo kampuni hiyo ni walipa kodi wakubwa wa Taifa.

Mwenyekiti wa Bodi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bw. Leonard Mususa akizungumza na wanahisa wakati wa hafla ya Mkutano Mkuu wa 51 wa mwaka wa Kampuni hiyo ambao ulifanyika jana kwenye kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.Mkutano huo uliangazia utendaji wa kifedha wa TBL PLC, mikakati na nafasi yake katika soko. Kushoto ni Katibu wa Kampuni Bi. Esther Kuja na kulia ni Mjumbe wa Bodi Bw. Phocus J. I. Lasway.