Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Kampuni ya identy inayoshiriki maonesho ya Fintech Festival Tanzania 2023 imekuja na teknolojia ya kisasa ambayo inawezesha kamera ya simu yeyote kutumika kutambua alama za kibiometrikia (Biometrics), Teknolojia hii adimu duniani inawezesha taasisi za kifedha na sekta nyingine katika nchi kuongeza usalama zaidi na kuzuia uhalifu kwa kuweza kuwahakiki watu kwa kutumia alama zao za vidole au sura kwa kupiga picha viganja vyao vya mikono au nyuso zao.
Akifafanua katika maonesho haya kampuni za teknolojia, Mkurugenzi wa identy Bw. Antony Vendah amekiri kwamba kampuni hii imewezesha nchi mbalimbali kukabiliana na changamoto kadhaa za kiuhalifu wa mtandao, ikiwa ni kwa kutumia mfumo huu ambo unaweza kutumia simu kumtambua mtu popote alipo. Amefafanua kwamba, Tassisi za kifedha hasa benki nchini, bado yanauhitaji wa teknolojia hii ili kupunguza muda unaotumika kufungua akaunti kwani kwa mfumo huu ndani ya sekunde 3 unaweza kuhakiki taarifa za mteja na kumfungulia akaunti.
Pia amekiri kua mfumo huu husaidia taasisi zinazotoa misaada kwa jamii, au tassisi za kilimo ili kuhakiki wanufaika kwa picha au alama za vidole,
Bw. Antony amesema kwa Tanzania wameweka mfumo huu kwenye benki kama CRDB, TCB, Exim, na Kampuni ya simu ya Vodacom na wanaendelea kuyakaribisha kampuni, taasisi za kifedha na wadau wengine kuungana nao.
Barani Afrika mfumo huu unatumika na nchi ya Ghana, South Africa, Nigeria na Tanzania
Banda la Identy limeendelea kuwa kivutio katika maonesho haya kutokana na umahiri wa Teknolojia hii na pia upekee wake kwani imeonekana kuwa suluhu la uhakiki na utambuzi wa taarifa binafsi.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa