June 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kampuni ya Heinken yafanya manunuzi ya Kampuni ya Distell,NBL

Na Penina Malundo, Timesmajira

MENEJA Mkazi nchini wa Kampuni ya Heinken , Obabiya Fagade amesema kampuni ya Heinken imefanya ununuzi wa Kampuni ya Distell Group Holdings(‘Distell’) na Kampuni ya Namibia Breweries (‘NBL’) ambapo ununuzi huo unafikia zaidi ya Euro Bilioni 1 katika mapato halisi.

Pia amesema ununuzi huo umefikia Euro milioni 150 katika faida ya uendeshaji wa nyayo zao za Afrika ambapo utachangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi nchini Tanzania.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaa,Fagade amesema wamepewa nafasi pekee kufikia hadhira pana zaidi kutokana na upanuzi wa kazi zao kutokana na ununuzi wa Kampuni hizo.

”Kampuni inayoongoza duniani ya kutengeneza Vinywaji Heineken inatarajia kuzindua rasmi jalada na chapa ya kampuni mpya ya aina mbalimbali itazinduliwa Mei 25 mwaka huu, kufuatia kukamilika kwa ununuzi wa kampuni hizo mbili za Dstell na NBL,”amesema

Amesema heineken kwa sasa inapatikana katika masoko 114 na kuuzwa katika zaidi ya masoko 180 na iko tayari kuwa kiongozi wa soko katika tasnia ya vnywaji nchini Tanzania.

Kwa upande wake Mkuu wa Biashara na Masoko ya Kampuni hiyo,Lilian Pascal ,amesema tangu mwaka 1864 wamekuwa wakisambaza bidhaa yao ya heineken na kufika katika mataifa mbalimbali.

Amesema katika kuwekeza nchini Tanzania Kampuni imeendelea kuamini sera za uwekezaji wa Tanzania na uwepo wa mazingira salama chini ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kukuza Chapa yao.

”Ushindani upo katika biashara yoyote,sisi tunatoa bidhaa yetu iliyobora na iliyokidhi vigezo na ndio maana hadi leo tupo katika soko muda mrefu,”amesema.