Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online, Dodoma
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Kampuni ya BARRON GROUP Jacqueline Kawishe.
Mazungumzo hayo yamefanyika Juni 30 mwaka huu , 2022 baada ya kufika kwenye ofisini za Spika wa Bunge Mjini Dodoma kwa lengo la kwenda kujitambulisha na kupata ushauri wa Spika hasa kwa kutambua mchango wa Bunge katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya sekta ya uwekezaji.
Akiwa na Spika huyo wa Bunge pamoja na mambo mengine Mkurugenzi wa Kampuni ya BARRON GROUP inajihusisha na utengenezaji na utengenezaji na uuzaji wa kiatu cha mtoto wa Shule chenye chapa ya kitanzania ya BARRON, Kawishe ameelezea sababu za kuamua kutengeneza kiatu cha mtoto wa shule ambacho ni bora na kwa gharama nafuu.
“Mheshimiwa Spika wa Bunge letu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo tumefika ofisini kwako kwanza kujitambulisha kuwa sisi BARRON GROUP ni kampuni ya Kitanzani iliyoamua kujikita katika kutengeneza kiatu cha mtoto wa shule.
“Tulifanya utafiti na kubaini kiatu cha shule kimekuwa changamoto kwa wazazi na walezi wengi, viatu vya shule vimekuwa na gharama lakini kwa sehemu kubwa vimekosa ubora, sisi tumeamua kuja na kiatu bora na kwa gharama nafuu,”amesema Kawishe.
Mkurugenzi huyo BARRON GROUP akiwa kwa Spika wa Bunge alikuwa ameambatana na Balozi wa kiatu hicho Nasikiwa Byera ambapo pamoja na kujitambulisha wamekabishi viatu vya shule jozi 50 kwa ajili ya Taasisi ya Tulia Trust Foundation.
More Stories
Tanzania Mwenyeji wa Mkutano wa nchi zinazozalisha kahawa Afrika
Watatu mbaroni kwa tuhuma za mauaji wakigombania shamba
Ng’ombe 10 wamekufa kwa kupigwa na radi