Na Judith Ferdinand, TimesMajira Online, Mwanza
Mkoa wa Mwanza umezindua kampeni ya kupunguza changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa inayoitwa ‘ uzalendo kwanza kazi iendelee.
Lengo ikiwa ni kuhakikisha wanafunzi wanasoma kwenye mazingira rafiki na salama na kupunguza mrundikano darasani.
Akizungumza kwenye uzinduzi huo uliofanyika katika Kijiji cha Mbela wilayani Misungwi
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel, ameeleza kuwa kampeni hiyo ya kupunguza changamoto ya upungufu wa madarasa ina thamani ya bilioni 238.08.
Mhandisi Robert, ameeleza kuwa watanzania wanapaswa kuwa wazalendo kwa kusaidia shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kuchimba msingi, kusomba mawe ili kuweza kupunguza gharama zitakazosaidia katika kutekeleza shughuli mbalimbali za kimaendeleo.
Kwa upande wake Mbunge Viti maalumu Mkoa wa Mwanza Kabula Shitobelo, ameeleza kuwa kupitia kampeni hiyo atasaidia tofali 400 kwa kila Wilaya.
“Zitasaidia kupunguza changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa kwani wazazi wamekuwa na mwitikio mkubwa wa kuwapeleka watoto wao shule hivyo kufanya idadi ya wanafunzi kuwa kubwa ukilinganisha na vyumba vya madarasa vilivyopo,”Kabula.
Naye Mbunge wa Jimbo la Misungwi Alexander Mnyeti amechangia kiasi cha milioni 20 kwaajili ya kuunga mkono ujenzi wa vyumba 25 vya madarasa katika shule ya mbtela.
“Shule ya Mbela ina watoto wengi kuliko shule zote zilizoko kwenye wilaya hii ina uwezo wa kubeba wanafunzi 800 lakini idadi ya wanafunzi waliopo ni 2000 hivyo ujenzi wa madarasa hayo yatakuwa suluhisho la kudumu na itasaidia wanafunzi kusoma vizuri,”.
Mkuu wa wilaya ya Misungwi Veronica Kessy, amewaomba wananchi kuendelea kujitolea katika kufanya kazi za kimaendeleo hali itakayosaidia watoto kusoma katika mazingira mazuri na hatimae kutimiza ndoto zao.
More Stories
Amos Lengael Nnko afariki kwa ajali ya gari
Gridi za Tanzania, Kenya kuimarisha upatikanaji wa umeme
Mama Zainab:Watoto yatima ni jukumu la jamii yote