December 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kampeni ya Sako kwa Bako yawafikia Kanda ya Kati

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma

Afisa Mkuu wa Biashara wa Kampuni ya Mtandao wa Tigo Tanzania Isaac Nchunda amesema kampuni hiyo ni moja ya mitandao inayokua kwa kasi na hivyo kurahisisha maisha ya watanzania .

Akizungumza katika ofisi za Tigo jijini Dodoma na waandishi wa habari, leo Agosti Mosi,2024 Nchunda amesema katika kuhakikisha kampuni ya Tigo inaendelea kurahisisha maisha ,imepeleka kampeni ya Sako kwa Bako Kanda ya Kati ambayo sasa ina miezi miwili tangu ianzishwe.

“Leo tigo ipo kanda ya kati na tumewaletea kampeni ya Sako kwa Bako  ambayo sasa ina miezi miwili, ikiwa Kanda ya kati Dodoma Makao Makuu ya nchi na ni siku nzuri ambayo usafiri wa reli ya mwendokasi (SGR) imezinduliwa ,tigo ndiyo mtandao bora zaidi Tanzania kwa sababu tuna teknolojia ya karne ya hivi sasa ya 4G na 5G ,

“Na hapa Dodoma tunayo 5G hivyo tunatoa huduma nzuri kwa wateja wanaotumia mtandao wa Tigo ambapo wanafurahia huduma yenye kasi zaidi ya 5G.”amesema Isaac

Amesema Sako Kwa Bako inatoa bonasi kwa kila mteja  anayenunua bando la tigo anapata MB na dakika za bure.

Amewaasa wananchi wajiunge zaidi na mtandao huo ili wanaufaike na ofa hizo ambapo pia ameizungumzia kampeni yao kupitia simu aina ya ZTE A34 ambapo amesema hiyo ni simu ya kisasa na inapatika kwa unafuu zaidi.

“Simu hii inauzwa shilingi  180,000 lakini pia inatolewa kwa mkopo ambapo mteja atatanguliza kiwango cha awali cha sh.35,000 na sh.650 kwa siku hadi mteja atakapomaliza deni lake na wakati huo huo wanaendelea kutumia simu yake kabla hata ya kumaliza deni lake.”amesisitiza

Akizungumzia kuhusu huduma za tigo kwa ujumla amesema ,kampuni hiyo inahudumia wateja zaidi ya milioni 21 huku akisema hiyo ni kwa sababu ya ubora wake.

“Takwimu hizo ni kwa mujibu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) na kwamba Tigo ndiyo mtandao unaokua kwa kasi zaidi nchini. “Amesema

Awali Mkurugenzi wa Kampuni ya Tigo Kanda ya Kati Said Iddy amesema kufuatia umuhimu wa uwepo wa Reli ya SGR ,amewaasa wananchi kutumia mtandao wa Tigo kwa ajili ya kukata tiketi ya treni hiyo.

Amesema kampuni hiyo imefanya maboresho makubwa ya mtandao wake kwa ajili ya kuboresha mtandao na biashara kwa ujumla kwa kutumia mtandao wa tigo kwa ajili ya kurahisisha maisha.

Pia amesema Tigo inashiriki maonesho ya wakulima na wafugaji (88 ) ambayo kitaifa yanafanyika mkoani Dodoma viwanja vya Nzuguni huku akiwasihi wananchi wote kutembelea banda la tigo kupata huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo.