Na David John, TimesMajira Online
MBUNGE wa jimbo la Ludewa Mkoani Njombe Joseph Kamonga, kwa mara ya kwanza ameshuhudia kuapishwa kwa Baraza jipya la Madiwani na ufunguzi wa baraza hilo huku Wise Mgina akichaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Halmashauri hiyo.
Akizungumza mara baada ya kupewa nafasi na mkuu wa mkoa wa Njombe Mwita Rubrya ambaye alishiriki katika uzinduzi huo wa baraza jipya la madiwani, Kamonga amempongeza Rais Dkt John Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya na kubwa ambalo amefurahishwa nalo alipowaapisha Mawaziri na Manaibu amesema, watu wanakuja kuwekeza kwenye upande wa chuma wapewe maeneo haraka na ikiwezekana wapewe hata bure.
Mbunge huyo, alifurahishwa na ya rais kwasababu katika jimbo lake la Ludewa kuna madini mengi ya chuma ambayo kimsingi ndiyo yanatumika kwenye kuzalisha chuma, hivyo anaiomba serikali kuja kuwekeza wilayani humo.
“Sisi sote nimashahidi, Ludewa katika nchi yetu ndio kuna madini mengi ya chuma kama Liganga. Lakini tuna makaa ya mawe eneo la mchuchuma na pia kuna madini aina ya chokaa nifursa kubwa tunayo na tunakuomba mkuu wa mkoa tufikishie salamu hizi,” amesema Kamonga
Akizungumza zaidi kwenye baraza hilo, Kamonga amewataka watalaamu na watumishi wa serikali ndani ya halmashauri hiyo kushirikiana naye kwani yeye alikuwa kwenye idara mbalimbali za utumishi hivyo yupo kwa ajili ya kuwatumikia wananchi na simu zake zipo wazi wakati wote.
“Mkurugenzi nakupongeza sana, kwani umejitahidi kukusanya mapato kwenye halmashauri yetu na tangu umefika kila mwaka mapato ya halmashauri yetu yanazidi kuongezeka, umeniambia kwaamba mwaka ujao umepanga kukusanya zaidi ya bilioni moja. Hadi sasa katika kipindi cha nusu mwaka umeweza kukusanya asilimia 55 ya mapato na umenihakikishia kwamba lengo ni bilioni moja hivyo nakupongeza sana kwakweli unafanya kazi kubwa,”amesema Kamonga
Ameongeza kuwa yeye na Mbunge wa viti malaumu balozi Pindi Chana watashirikiana kwa pamoja kuhakikisha kwa pamoja wanajenga Ludewa .
Naye katibu tawala Zaina Mlawa aliwaeleza madiwani wa upinzani kwamba kwakuwa wamechaguliwa kuwa madiwani wajuwe kuwa wanatekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi huku akiwataka madiwnai wateule kwenda kushirikiana na watendaji kata lakini pia kuwa na maadili katika uongozi wao kwani ni kioo cha jamii.
More Stories
RC.Makongoro ataka miradi itekelezwe kwa viwango
LALJI yatoa msaada wa sare na vifaa vya shule kwa yatima
Dkt.Biteko aagiza Kituo cha huduma kwa wateja Tanesco kusukwa upya