Na David John, TimesMajira Online
MBUNGE wa Jimbo la Ludewa mkoani Njombe, Wakili Joseph Kamonga amegawa seti za jenzi na mipira 35 kwenye vijiji 77 vilivyopo Wilayani humo kwa lengo la kuinua michezo jimboni mwake huku akiwataka vijana kwenda kutumia vizuri vifaa hivyo.
Akizungumza mbele ya wananchi na viongozi mbalimbali wa Halmashauri hiyo ambapo kabla ya kuaza kugawa jenzi ilitanguliwa na mechi ya kirafiki kati ya Madiwani na watumishi wa Halmashauri na katika mchezo huo Madiwani waliibuka kidedea kwa ushindi wa goli 1-0.
Wakati akipita kuomba kura kwa wananchi, moja ya ahadi yake ilikuwa ni lazima vijana kuibua vipaji vyao katika michezo ili mwisho wa siku kujiariji na ndio sababu iliyomsukuma kutoa vifaa hivyo.
“Ndugu zangu nimeona nitumie mchezo huu kati ya Madiwani wetu na watumishi kugawa jenzi hizi na kwa kuanzia nimeaza kutoa jezi wa Kata tano ambazo ni Ludewa mjini, Lupingu, Luaga, Ludenda Nkoma Ng’ombe na baadae zoezi hilo litaendelea kwa vijana waliosalia ili baadaye iwe rahisi kwao kucheza Ligi, kwani katika ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) inazungumzia michezo na mimi kwenye Kampeni zangu niliahidi vijana kuwapelekea vifaa vya michezo ikiwamo mipara, “.
“Pia nawaomba Madiwani nendeni mkasimamie vizuri usimamizi wa vifaa kwani kufanya vizuri kwangu ndio kufanya vizuri kwenu, kikubwa ni kushirikiana kutimiza lengo la kuibua vipaji na kuona wanapatikana akina Thomas Masaki wengine, ” amesema Kamonga.
More Stories
Zanzibar kuzalisha wachezaji wenye vipaji
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes
Rais Samia: Yanga endeleeni kuipeperusha bendera ya Tanzania