March 13, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kamishna wa Zimamoto atoa pole kwa waathirika wa majanga ya moto

KAMISHNA WA ZIMA MOTO ATOA POLE KWA WALIOATHIRIKA

Na Bakari Lulela 

KAMISHNA wa jeshi la zima moto na uokoaji Kanda maalumu ya Dar es salaam Peter Mtui ametoa pole na tahadhari kwa wakazi wa Mkunduge dhidi ya majanga ya moto yanayotokea kwenye malazi ya watu.

Akizungumza jijini Dar es salaam hivi karibuni kufuatia mwaliko wake kwa mwenyekiti wa serikali ya mitaa wa Mkunduge Saidi Mrisho mara alipotembelea ofisi kwake jijini Dar es salaam.

“Pole sana mwenyekiti kwa madhila yaliyokupata kwa wakaazi wako, sisi kikosi cha zimamoto na uokoaji tuko pamoja na waathirika wa janga la moto lililotokea 28 januari 2025 katika mtaa wa Mkunduge,” amesema Kamishna

Aidha Kamishna huyo amesema kuwa kikosi cha zimamoto na uokoaji kinajukumu la kufuatilia kinapata Taarifa za uhakika Ili kuendelea kutoa huduma stahili za zuia ama kuzima moto kwa wakati unaotokana na matatizo mbalimbali yaliyomo ndani ya jamii kwa ujumla.

Kwa upande wake mwenyekiti huyo Said Mrisho amesema kwamba anapokea pole hizo kwa ajili ya wakaazi walioathirika na janga lile na kuahidi kuendelea kuyasimamia sera na majukumu ya serikali katika kuwahudumia wananchi wa Mkunduge wakati wa majanga ama matukio mbalimbali .