December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kamishna Mkuu TRA akutana na kufanya mazungumzo na Waziri Yu Jianhua

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Yusuph Mwenda Agosti 14. 2024 amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mamlaka ya Forodha ya Jamhuri ya Watu wa China, Yu Jianhua aliyetembelea katika ofisi yake, jijini Dar es Salaam.

Mazungumzo hayo yaliambatana na utiaji saini wa makubaliano ya kukuza uhusiano baina ya Tanzania na China katika masuala ya Forodha.