Na Esther Macha,TimesmajiraOnline , Chunya
WAJUMBE wa kamati zote zinazojishghulisha na ujenzi wametakiwa kujengewa uwezo wa kusimamia miradi mbalimbali ya ujenzi kabla ya kukabidhiwa majukumu ya miradi ili wakikiuka utaratibu waweze kuchukuliwa hatua kwa haki na kwa mujibu wa kanuni na miongozo.
Wito huo umetolewa leo na Mkuu wa wilaya ya Chunya mkoani Mbeya, Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji Mbaraka Alhaji Batenga wakati alipofanya ziara ya kukagua mradi wa Zahanati ya Igundu ambao umegharimu zaidi ya milioni hamsini (50,000,000) ambazo zimepelekwa kujenga miundombinu mbalimbali ikiwepo tanki la maji, vinawia mikono, vyoo na kichomea taka
“Wajumbe wote wa kamati za ujenzi wajengewe uwezo wa kusimamia miradi hiyo kabla ya kukabidhiwa jukumu la kuanza kusimamia mradi husika jambo ambalo litasaidia wajumbe hao kusimamia ipasavyo mradi husika na hata kuhakikisha ukamilifu wa mradi huo” amesema Batenga
Aidha Mhe Batenga ameuagiza uongozi wa Afya kuzingatia ushauri uliotolewa na Wakala wa maji na Usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) pamoja na TANESCO ili kuhakikisha wananchi wa Igundu wanaendelee kutatua changamoto zote maana hilo ndio lengo la Serikali kusogeza miradi mbalimbali kwa wananchi wake wakiwepo wananchi wa wilaya ya Chunya
Kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya, Kaimu Mganga Mkuu Edward Tengulaga amesema siku saba zinatosha kuhakikisha kibao kinachoonesha huduma zinazotolewa katika zahanati hiyo kinawekwa pamoja na kibao kinachoonesha uwepo wa Zahanati eneo hilo vitu ambavyo vilibainishwa kwamba ni muhimu na havikuwepo ili kuwarahishisia wananchi ambao sio wenyeji watakapohitaji huduma hiyo
Ziara ya Mkuu wa wilaya ililenga kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa katika kata ya Sangambi ambapo alitembelea pia mradi wa Maji Igundu, mradi wa ujenzi wa vyoo katika Shule ya msingi Sangambi, mradi wa ujenzi wa kituo cha Afya pamoja na kukagua hali ya mazingira katika kitongoji cha Tukuyu.
More Stories
Prof. Mwakalila asisitiza uadilifu, uzalendo kwa wanafunzi wapya chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere
Benki ya Equity Tanzania yasaini mkataba wa kuwawezesha wanawake kiuchumi
Rais Samia alivyoguswa kifo cha msanii Grace Mapunda