Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online
Wananchi Katika Eneo la Mvomero mkoani Morogoro wamemwambia Waziri Gwajima kuwa hawazijui kamati ya ulinzi wa wanawake na watoto wa Kata za eneo hilo
Wananchi hao wa Kata ya Dakawa Wametoa kilio chao kwa Waziri Dkt. Gwajima Desemba 04, 2022 aliye lazimika kusimama na kuzungumza na wananchi wa eneo hilo akiwa katika Ziara ya Ufuatiliaji wa Kampeni ya Siu 16 za Kupinga Ukatili.
Kufuatia hali hiyo, Waziri Dkt. Gwajima ametoa maelekezo kwa Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya hiyo Sia kuhakikisha kamati hizo zinafuata mwongozo wa uanzishwaji na uendeshaji wake. MTAKUWWA
Aidha ameutaka uongozi wa Kata husika kuhakikisha wananchi wanapewa elimu ya kutosha katika siku hizi za Kampeni na baada ya Kampeni kwa kushirikiana na wadau wote wanaohusika na kupinga ukatili wilayani humo.
Waziri Gwajima aliendelea kusisitiza wanaume kujitokeza kushiriki kampeni ya kupinga ukatili kwa nguvu zote.
Kuanzia Desemba 04,2022 Waziri Dkt. Gwajima amepita Mikoa ya Morogoro, Dodoma, Singida akielkea hadi Mara akitoa Elimu kwakutumia Vituo.vya Redio na Kuzungumza na Wananchi katika Maeneo anayopita kwenye Mikoa hiyo.
More Stories
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu