April 1, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kamati ya usalama barabarani yakabidhi vitendea kazi kwa jeshi la polisi Mbeya

Na Esther Macha,TimesmajiraOnline,Mbeya

KAMATI ya usalama barabarani mkoa wa Mbeya imekabidhi vitendea kazi vya ofisi ikiwemo kompyuta na Photocopy Machine  kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya ili viweze kusaidia jitihada kuzuia ajali

Akikabidhi msaada huo leo Machi 29,2025  katika uwanja wa mazoezi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia Mbeya  Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama barabarani Mkoani humo ,Mhandisi Rajabu Ghuliku amesema kuwa msaada huo unalenga kurahisisha utendaji kazi na kuleta ufanisi katika jitihada za kuzuia na kudhibiti ajali za barabarani.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya,Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Benjamin Kuzaga amewataka Wakuu wa Polisi Wilaya zote za Mkoa wa Mbeya kutunza vitendea kazi hivyo na kuhakikisha vinatumika vizuri ili kuleta matokeo chanya katika kuzuia na kudhibiti ajali za barabarani.

Aidha,Kamanda Kuzaga ameishukuru Kamati hiyo kwa vitendea kazi hivyo kwani kutokana na ukuaji wa matumizi ya TEHAMA ikiwemo mifumo ya kidigitali ya utendaji kazi ndani ya Jeshi la Polisi ni wazi kuwa vifaa hivyo vinakwenda kuongeza tija na weledi katika utendaji kazi.

“Tunashukuru kwa vifaa hivi vitakwenda kusaidia utendaji kazi wa jeshi polisi kitengo cha usalama barabarani kwa ufanisi mkubwa katika kuthibiti ajali,” amesema Kamanda Kuzaga.

Naye, Mkuu wa Kikosi cha usalama barabarani mkoani Mbeya ambaye pia ni Katibu wa Kamati ya Usalama barabarani Mkoa, SP Notker Kilewa amesema kuwa msaada huo unakwenda kuongeza weledi katika utendaji kazi za kikosi hicho na kutoa shukrani kwa kamati kuweza kutoa kompyuta za mezani saba na “heavy duty photocopy machine.