Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
DIWANI Paschal Raina Linyamala ,wa kata ya Majohe wilayani Ilala na Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi( CCM) kata ya Majohe wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan, kwa kuwekeza miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo sekta ya afya na sekta ya Elimu.
Diwani Paschal na Kamati yake ya siasa alisema hayo wakati wa ziara ya Kamati ya siasa kukagua miradi ya maendeleo iliyotekekezwa na Serikali katika miaka mitatu ya Dkt.Samia Suluhu Hassan.
“Tunampongeza Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika uongozi wake wa miaka mitatu kata ya Majohe amefanya mambo makubwa ikiwemo utekelezaji wa Ilani ambapo Serikali imejenga kituo cha afya cha kisasa,shule za msingi na sekondari tunajivunia uongozi wa Dkt.Samia kwa miradi mikubwa ya maendeleo “alisema Paschal.
Diwani Paschal alisema katika kata ya majohe awali kulikuwa na zahanati kwa sasa zahanati hiyo imepandishwa hadhi na kujengwa kituo cha afya cha Kisasa ambacho kinatoa huduma kwa wananchi wa eneo hilo na kata za jirani .
Alisema kituo hicho cha afya kimejengwa majengo matatu likiwemo wodi ya wanawake kwa ajili ya kujifungulia kwa sasa wamama wajawazito wanatumia kituo hicho cha afya awali walikuwa wakikiimbilia Wilaya ya Kisarawe na Pugu kwa ajili ya kufuata huduma za afya kubwa.
Katika ziara hiyo ya Kamati ya Siasa ya chama cha Mapinduzi Majohe walitembelea kuangalia miundombinu ya Barabara na madaraja ambayo yanajengwa na Serikali katika uongozi wa Dkt.Samia Suluhu Hassan ambapo Diwani Paschal aliwataka wananchi kuvuta subira Serikali ni sikivu imesikia changamoto za Barabara hivi karibuni zinajengwa na mradi wa DMDP.
Pia walitembelea shule za msingi na sekondari zilizopo Kata ya Majohe ikiwemo Viwenge shule ya Sekondari na shule ya Msingi,Kichangani ,Shule ya Uamuzi,na Harisi Sekondari kuangalia utekelezaji wa Ilani ambapo Serikali imetoa pesa kwa ajili ya madarasa mapya na kuboresha miundombinu ya shule hizo.
Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Majohe Nuru Mwalimu Mizumo alipongeza Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan Mbunge wa jimbo la Ukonga Jery Silaa na Diwani wa Majohe Paschal Linyamala kwa utekelezaji wa Ilani ya chama vizuri ambapo alisema miradi hiyo ya Serikali Majohe imekuwa ya kisasa zaidi kata hiyo ina shule za kutosha na Kituo cha afya cha kisasa.
Mwenyekiti Nuru Mwalimu alisema kitendo cha Serikali kusogeza huduma za afya sasa hivi wanajivunia wamama wajawazito hawapati usumbufu wa kusaka matibabu mbali.
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi Majohe Denice Pachaley alisema kituo cha afya Majohe jengo hilo lilianza kutoa huduma Mwezi Machi 2024 ambapo mpaka sasa Jumla ya watoto waliozaliwa katika kituo hicho 63 Changamoto iliyokuwemo Wamama wajawazito kujifungua njiani kutokana na Barabara mbovu Majohe
More Stories
Bodaboda wamchangia Rais Samia Mil 1 ya fomu ya Urais
HAYA HAPA MATOKEO YOTE FORM II NA DARASA LA IV
Ufaulu waongezeka matokeo ya Darasa la Nne na Kidato cha Pili